Na Mwandishi Wetu,Hanang
CHAMA
Chama Mapinduzi (CCM)kimesema kwamba vituo vyoye vya ambavyo vimejengwa
nchi nzima vitapelekewa dawa na vifaa tiba kwa lengo la kuhakikisha
vinatoa huduma za matibabu ya afya kama ambavyo imekusudiwa.
Akizungumza
leo Machi 5,2023 baada ya kutembelea Kituo cha afya Basotu kilichopo
wilayani Hanang mkoani Manyara Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo
amesema hadi ufikia Juni 2023, vituo vya afya vilivyojengwa nchi
vitapelekewa vifaa tiba.
Chongolo amesema tayari amewasiliana na
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akamweleza mpango wa serikali na Bohari Kuu
ya Dawa (MSD) wa kuagiza kwa jumla vifaa tiba vitakavyosambazwa nchi
nzima kwenye vituo vya afya,lengo kuhakikisha wananchi wanapata huduma.
Amesisitiza
watahakikisha vituo vyote vya afya vinapata vifaa tiba kwani hawawezi
kuwa na majengo mazuri lakini hayana huduma,hivyo Chama hicho
kinachotaka kuona ni huduma bora zinatolewa ambazo zitaendana na uzuri
wa majengo hayo.
"Serikali imejikita kwenye ujenzi wa vituo vya
afya ili kutoa huduma ya afya ya uzazi salama kwa mama na mtoto sambamba
na kupunguza vifo vyao hadi kufikia asilimia 0.Hivyo moja wajibu Wetu
kama Chama ni kusimamia malengo hayo."
Chongolo wakati anaanza
kuzungumza ameipongeza pia Halmashauri ya Hanang kwa kutenga fedha kwa
ajili ya ujenzi wa kituo hicho kwa kutumia makusanyo ya ndani,majengo
mazuri,yanavutia.
"Wamefanya hivi kwanini kwasababu Serikali Kuu
imefanya kazi kubwa zifuatazo ndani ya Halmashauri ya Hanang ikiwemo
kubeba jukumu la mishahara yote ya watumishi fedha zinatoka Serikali
Kuu.
"Pia Serikali imeweka mpango kwa halmashauri ambazo uwezo
uko chini asilimia 40 ya makusanyo ya ndani yanatakiwa kwenda kwenye
miradi na halmashauri ambazo ziko juu asilimia 60 ya makusanyo inakwenda
kwenye maendeleo."
Awali,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Dk
Mohamed Nkodi ameeleza kwamba zahanati ya Basutu ilijengwa mwaka 1999 na
ilipofika mwaka 2006 ilipandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya.
"Kituo
hiki hakikutengewa fedha kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya majengo
hadi kilipotengewa Sh.milioni 400 katika bajeti ya mwaka 2021/22.Ujenzi
wa kituo hiki kimekamilika kwa asilimia 99, kilichobaki ni kupata vifaa
tiba kwa ajili ya chumba cha upasuaji."
Katibu Mkuu wa ChamaCha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama wa CCM na wakazi wa Hanang mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Basotu, Hanang mkoani Mara.
Sehemu ya wanachama wa CCM na wakazi wa Basotu waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ambaye pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa walifika Basotu na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Basotu.
No comments:
Post a Comment