HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 7, 2023

Halotel yaunga mkono kampeni uchangiaji damu shuleni Kisutu

 Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuokoa maisha ya wagonjwa wanahitaji damu, kampuni ya simu ya Halotel leo tarehe 6, Machi, 2023 imeshirikiana na imeungana Shule ya Sekondari ya Wasichana na Taasisi ya Mifupa (MOI) kuandaa tukio kubwa la uchangiaji damu kwa hiari.


Zoezi hili litawajumuisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za shule kutoka mkoani Dar Salaam.

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani mnamo tarehe 8 Machi ya kila mwaka, Halotel imeina ni muhimu kusherehekea siku hiyo kwa kuchangia katika sekta ya afya katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta hiyo kwa maendeleo ya nchi.

Halotel kwa kushirikiana na MOI imewezesha utekelezaji wa kampeni ya uchangiaji damu chini ya shule ya sekondari Kisutu kwa kuchangia vifaa mbalimbali ikiwemo Tisheti, chakula, vinywaji na vitafunwa kwa ajili ya kutumika wakati wa zoezi la uchangiaji damu litakalofanyika siku ya tarehe 06/03/2023 katika viwanja vya shule ya sekondari Kisutu jijini Dar Es Salaam.

Akiongea katika tukio la kukabidhi vifaa hivyo, Mkuu wa kitengo cha masoko Halotel, Bi Sakina Makabu amesema: " Hii ni katika kuhakikisha kwamba tunaipunguzia Serikali ya Awamu ya Sita mzigo katika kupunguza changamoto ya kukosekana kwa damu ya kutosha kuokoa maisha ya wagonjwa katika taaisisi ya MOI na hospitali ya Muhimbili."

Aliongeza: "Wajawazito, manusura wa ajali, watoto chini ya miaka mitano wapo katika kundi lenye uhitaji mkubwa wa damu, hivyo kuwezesha zoezi hili ni ishara ya upendo wa kampuni kwa Watanzania ambao pia ni wateja wake."

Zoezi hilo linatarajiwa kushirikisha zaidi ya shule 40 ambazo zitaleta wanafunzi zaidi ya 2000.

Kwa upande wake, Afisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi, taasisi imefurahishwa kwa mwitikio kutoka kampuni ya Halotel kwa kuwezesha kampeni ya Shule ya Sekondari Kisutu ya uchangiaji damu.

uchangiaji damu.

"Hii inaonesha namna kampuni inavyojali afya za wananchi na juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya afya. Hii ni hatua kubwa kwetu kuelekea kuimarisha zaidi uhusiano wetu na kampuni ya Halotel katika kuboresha sekta ya afya," Bw Mvungi amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisutu, Bi Chiku Mhando, ameishukuru Halotel kwa kuwa mdhamini wa tukio hilo muhimu, na akawaomba watu binafsi, makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kuunga mkono zoezi hilo ili kuongeza kiwango cha damu kwenye benki ya damu.

Sera ya Kampuni ya Halotel siyo tu imejikita kibiashara bali pia ni kusaidia jamii, kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia Serikali za kuboresha sekta ya afya na elimu.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel Sakina Makabu akikabidhi mahitaji na vifaa mbalimbali ikiwemo Tisheti, chakula, vinywaji na vitafunwa kwa Mkuu wa Shule ya wasichana ya Kisutu Bi Chiku Mhando kwa ajili ya kutumika wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika leo katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Kisutu jijini Dar es Salaam ili kuunga juhudi za serikali katika upatikanaji damu kwaajili ya wagonjwa mbalimbali katika hospital ya MOI na Muhimbili. Pamoja nao ni Afisa Kutoka MOI Bw. Joel Mushi (katikati) na wanafunzi mbalimbali kutoka shule hiyo


Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel Sakina Makabu akiongea na waandishi wa habari katika shule ya sekondari ya wasichana Kisutu iliyopo Dar es salaam leo wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika leo katika viwanja vya shule shule hiyo jijini Dar es Salaam ambapo Halotel illidhamini vifaa na mahitaji mbalimbali ikiwemo Tisheti, chakula, vinywaji ili kufanikisha na kuunga juhudi za serikali la upatikanaji damu kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji katika hospitali ya MOI na Muhimbili.






Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bw; Abdallah Salum akiambatana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Dr. Rashid Mfaume katika kampeni na zoezi la uchangiaji damu lililofanyika leo katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo Halotel waliwezesha zoezi hilo kwakudhamini mahitaji mbalimbali ikiwemo vinywaji na vyakula. Pamoja nao ni Meneja wa Kitengo cha Uhusiano MOI Patric Mvungi, Miss Tanzania 2022/2023 Halima Kopwe, Mkuu wa Shuke ya sekondari wasichana Kisutu Bi Chiku Mhando na wageni wengine waalikwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad