HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 5, 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Zaujia Swalehe (1) mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Usa River Mkoani Arusha. Kushoto ni Mama wa Mtoto huyo Bi. Ashura Mohamed Mkazi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha wakati akielekea KIA baada ya Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali, tarehe 05 Machi, 2023.
Wananchi wa Arumeru wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili Usa River Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wakazi Maarufu wa Arumeru Timoth Palangyo na Shedrack Palangyo mara baada ya kuhutubia Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.
Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wakiwa wameshika Mabango wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Usa River Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.


Msafara wa Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wa Jijini Arusha wakisindikiza Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akielekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali, tarehe 05 Machi, 2023.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad