Kaimu Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Monica Mutoni, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa warsha ya siku moja kuelekea Utabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei 2023). Warsha hiyo imefanyika Februari 21,2023 Kibaha mkoani Pwani.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini, Dkt. Ladislus Chang'a akizungumza na waandishi wa habari wakati ya warsha ya siku moja kwa wanahabari kuelekea Utabiri wa msimu wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei 2023). Warsha hiyo imefanyika Kibaha mkoani Pwani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA, Dkt. Pascal Waniha.
Baadhi ya Waandishi wa habari za mtandaoni, wakijadiliana namna ya kutoa taarifa za hali ya Hewa kwa jamii wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika leo Februari 21,2023 Kibaha mkoani Pwani. kuelekea Utabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei 2023) iliyofanyika Februari 21,2023 Kibaha mkoani Pwani.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika warsha ya siku moja kuelekea Utabiri wa msimu wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei 2023). Warsha hiyo imefanyika Kibaha mkoani Pwani Februari 21,2023
TMA yawapongeza wanahabari
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAMLAKA ya Hali ya hewa nchini (TMA) imewapongeza waandishi habari nchini kwa kuendelea kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wakati na kwa usahihi sambamba na kuelimisha jamii ili iweze kuepukana na majanga yanayoweza kutokea kwa hali mbaya ya hewa.
Pia imewaasa waandishi hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa jamii nzima ili kuhakikisha wanaendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa nchini ili kupata mapema tahadhari na taarifa za hali ya hewa na athari zake.
Hayo yamesemwa Februari 21, 2022, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini, Dkt. Ladislausi Changa wakati akifungua warsha ya siku moja kwa wanahabari kuelekea Utabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei 2023) iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani.
" Mmekuwa wanahabari na mabalozi wazuri sana kwa kutoa taarifa za TMA, ninawapongeza sana, nawasihi muendelee kufanya habari hizi ziwe bora zaidi leo kuliko jana na na kesho kuliko leo" amesema Dkt. Chan'ga.
Aidha Dkt. Chang'a amesema, uharibifu wa mazingira unaofanywa na jamii ikiwemo ukataji miti ovyo umekuwa ukipelekea joto la dunia kuongezeza ambapo kwa kipindi cha miaka mitano joto limeongezeka kwa asilimia 1.15 na linatarajiwa kuongezeka hadi kufikia asilimia 1.5 kufikia 2030.
"Ninaisa jamii kuchukua hatua mbali mbali kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi ili hali hiyo isiendelee ikiwemo kupunguza shughuli za kibinadamu zinazopelekea mabadiriko hayo kutokea" amesema
Dkt. Chang"a ameongeza kuwa, Mamlaka iko kwenye mikakati ya kuhakikisha wanaanza kutoa utabiri kwa maeneo madogo madogo ili kuwezesha jamii kupata taarifa za hali ya hewa katika maeneo yao.
Dkt. Chang’a amesema Kuongezeka kwa muamko na taarifa za hali ya hewa ni muhimu kutokana na changamoto za hali ya hewa duniani ambapo kwa sasa joto duniani linaongezeka ambapo kila mwaka joto duniani huongezeka ambapo inatarajiwa kufikia nyuzi joto 1.5 ifikapo mwaka 2030 kama jitihada za kupunguza ongezeko hilo la joto hazitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment