NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM)Balozi Rajab Luwhavi ameipongeza Jumuiya ya
Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuandaa mafunzo maalumu ya viongozi wa
jumuiya hiyo yaliyoanza kutolewa kwa Kamati ya utekelezaji.
Balozi
Luwhavi ametoa pongezi hizo leo Januari 13,2023 jijini Dar es Salaam
mbele ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyoratibiwa na jumuiya hiyo chini
ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Khadija Ally baada ya kutembelea Kambi ya
mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika Kigamboni,Jijini Dar es Salaam.
Amesema
kwamba amevutiwa na mafunzo hayo na yameonesha mwanzo mpya wa Jumuiya
ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwamua kuwapatia mafunzo hayo
viongozi wake.
“Nampongeza Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Dar es Salaam Khadija Ally kwa kuandaa mafunzo haya.Hakujipa muda wa
kusherehekea nafasi aliyoipata baada ya kuchaguliwa ameamua kuandaa
mafunzo hayo huku akitumia nafasi hiyo kukumbusha mambo ya msingi
yanayohusu Chama hicho na jumuiya zake'',amesma Balozi Luwahi.
Amesema
moja ya changamoto iliopo ni zana ya kuamini wanaopaswa kuelimishwa ni
wale walioko chini kabisa,la hasha huyu Mwenyekiti mmepata mpya kabisa
na maalum, ameanza kujifunza yeye na Kamati yake ya utendaji kwanza,na
kwamba anampongeza Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, kwa sababu mtazamo wake
sio mtazamo wa viongozi wa sasa .
''Mkoa wa Dar es Salaam ni
namba moja kwa kila kitu, namba moja kwa ukubwa wake maana ndio
unaongoza kwa idadi ya watu Tanzania, lakini ndio namba moja kwa nguvu
zake kiuchumi,ndio mlango mkubwa wa kupokea na kutoa wageni kwenye nchi
yetu, unapopata uongozi Mkoa wa Dar es Salaam ni tofauti na unapopata
uongozi katika mkoa mwingine,Kwanini ni kwasababu ya mazingira ya mkoa
wenyewe kwa hiyo nampongeza sana kwa mwanzo aliounesha wa kuandaa
mafunzo haya kwa kamati yake ya utekelezaji ''amesema Balozi Luwhavi.
“Nampongeza
yeye kwasababu hakujipa muda wa kusherehekea nafasi aliyoipata baada ya
kuchaguliwa, amekiwahi hata chama chenyewe, tuendelee kumuombea kwa
Mwenyezi Mungu aendelee kumpa nguvu na maarifa , afya njema na umri
mrefu zaidi ili atutumikie zaidi kwenye chama chetu, lakini niwapongeze
ninyi nyote kwa kuchaguliwa.
Kuhusu jumuiya ya wazazi amesema kwa
mujibu wa historia ndio jumuiya kubwa yenye lengo la kuwanganisha
wazazi wote na kuwa mwanachama wa jumuiya ya wazazi sio lazima uwe
mwanachama wa CCM.
“Katiba ya CCM haijawazuia kuwa mwanachama wa
CCM kama haujaingia kwenye jumuiya wala haijasema kwa mtu anayependa
kuwa mwanachama wa jumuiya ya wazazi peke yake akaridhika akawa
mwanachama wa CCM isipokuwa tu ukitaka kugombea uongozi utakaokuingiza
kwenye vikao vya Chama hicho basi sharti lake lazima uwe mwanachama wa
CCM.
” Ndio maana huko nyuma tulitenganisha suala la itikadi na
kuwaunganisha watu,kwasababu jukumu la kwanza la jumuiya ya wazazi ni
kuwaunganisha wazazi wote chini ya uongozi mmoja, jukumu lake la pili
ndio la kwenda kwenye uanachama.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally amewaomba waliopata
nafasi ya kushiriki kwenye mafunzo ya uongozi kuwa wasikivu ili nao
waweze kuacha alama bora na alama ya uongozi bora uliotukuka.“Tuwe
viongozi ambao tutaishi na hata tutakapokufa tutaacha alama na kuwa
mfano kwa wengine.
Aidha amesema kupitia mafunzo ya uongozi
yanayotolewa kwa viongozi hao kuna mambo mengi wamejifunza na washiriki
wameonesha kubeba yale yote yaliyoelezwa na wakufunzi huku akitumia
nafasi hiyo kueleza wameingia kwenye mafunzo hayo kama wajumbe lakini
watatoka kama viongozi .“Dhana ni ile ile ,Chama chetu ya Mapinduzi
kimekuwa tanuru la kutoa viongozi.”
NAIBU
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Rajab Luwhavi
akizungumza mbele ya Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa
Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
Januari 13,2023 katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es
Salaam,pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es
Salaam Khadija Ally akifuatilia kwa makini,kushoto ni Wakufunzi wa
Mafunzo hayo.Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Ally akizungumza
wakati akimkaribisha NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Balozi Rajab Luwhavi katika alipotembelea kambi ya mafunzo hayo
ya siku tatu kwa Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yanayoendelea katika
hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
NAIBU
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Rajab Luwhavi
akioneshwa Kadi ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa
wa Dar es Salaam Khadija Ally wakati wa Mafunzo yakiendelea.
Mmoja
wa Washiriki wa Mafunzo hayo akisoma baadhi ya Vifungu kwenye Katiba ya
CCM ikiwa ni sehemu ya kujengewa uwezo wa Uongozi wa Kamati hiyo Washiriki wakifuatilia kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa kwenye mafunzo hayo.
NAIBU
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Rajab Luwhavi
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa mafunzo pamoja na
Wakufunzi wa Mafunzo hayo.
NAIBU
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Rajab Luwhavi
akipokewa na Mwenyekiti wa Wazazi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Khadija
Ally mara baada ya kuwasili eneo la Mafunzo yanayofanyika kwa siku tatu
katika hotel ya Star Breeze iliyopo Mbutu Kigamboni kwa ajili ya
kuwafunda masuala mbalimbali ya Uongozi Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya
ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam.
Saturday, January 14, 2023

Home
SIASA
JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM YAPONGEZWA KUANDAA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WAKE
JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM YAPONGEZWA KUANDAA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment