Katika kusherekea maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar, wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoka matawi ya Zanzibar wameungana na Baraza la Udhibiti la Mifumo wa utoaii Leseni (BLRC) Zanzibar kufanya usafi Kwenye viwanja vya Maisara.
Hii
ikiwa ni ushiriki wao kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zilizopangwa
na serikali katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar.
Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa michuano ya kombe la Mapinduzi yatakayofanyika kesho uwanja wa Amaan.
Wafanyakazi
wa Benki ya NMB, Zanzibar pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Udhibiti
la Mifumo wa utoaji Leseni (BLRC) wakishiriki kufanya usafi wa viwanja
vya Maisara ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 59 ya
Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964.

Meneja wa Biashara za Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame (wapili kulia) pamoja na baadhi ya watumishi wa Benki ya NMB na Baraza la Udhibiti wa Mifumo ya utoaji Leseni (BLRC) Zanzibar wakiwa katika shuguli za kuvisafisha viwanja vya maisaraikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi matakatifu ya Zanzibar.

No comments:
Post a Comment