Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation Bi. Caren Rowland akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya young scientist tanzania (yst), Gozibert kamugisha akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kumekuwa na muamko mkubwa wa wanafunzi kujihusisha na tafiti za kisayansi na ugunduzi nchini ambapo kwa mwaka 2022 wanafunzi takribani 1143 wamewasilisha maombi ya kufanya kazi hizo ambapo kati yao tafiti 530 zimepatiwa usaidizi na hatimaye kazi 380 zimekamilika mpaka sasa.
WAMILIKI wa viwanda, Wazazi, Walimu na Jamii kwa ujumla wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuwawezesha vijana wanaojihusisha na gunduzi na tafiti za kisayansi ili kuziendeleza tafiti hizo hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji sambamba na kupunguza garama za uzalishaji kupitia teknolojia zinazobuniwa ndani ya nchi.
Hayo yamesemwa na mwanzilishi mwenza wa taasisi ya young scientist tanzania (yst) Gozibert kamugisha wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kuongeza kuwa kumekuwa na muamko mkubwa wa wanafunzi kujihusisha na tafiti za kisayansi na ugunduzi nchini ambapo kwa mwaka 2022 wanafunzi takribani 1143 wamewasilisha maombi ya kufanya kazi hizo ambapo kati yao tafiti 530 zimepatiwa usaidizi na hatimaye kazi 380 zimekamilika mpaka sasa
Aidha amebainisha kuwa baadhi ya kazi za kisayasi zitakazoonyeshwa kwenye maonyesho ya mwaka huu zimejikita katika masuala ya utunzaji wa mazao ya kilimo, utunzaji wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali maji, uzalishaji wa umeme, kuboresha uzalushaji wa maziwa ya ngombe na kutatua tatizo la udumavu wa kuku.
kwa upande wake afisa mtendaji wa taasisi ya karimjee jivanjee Caren Rowland amesema kuwa mpaka kufikia mwaka 2021 taasisi yao imefanikisha kusaidia vijana wapatao 37 na pia inatarajia kupata washindi wengine wanne watakaopatikana katika mashindano ya mwaka huu na kufikia idadi ya vijana 41 huku akiongeza kuwa taasisi yao imejitolea kuunda mustakabali mzuri kwa vijana wa kitanzania kupitia elimu na uwezeshaji ili kuendeleza kizazi kijacho cha viongozi watakaochagiza mabadiliko endelevu kwa Tanzania na dunia kwa ujumla
Maonyesho hayo kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika disemba 8 katika hoteli ya serena jijini dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa waziri wa elimu, sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Mwanzilishi Mwenza wa Young Scientists Tanzania (YST) Dkt.Gozibert Kamugisha Akizungumza na waandishi wa habari Leo Desemba 4,2022 Jinini Dar es salaam Kuelekea maonesho ya YST yatakayofanyika Desemba 8,2022 kwenye hotel ya serena jijini Dar es salaam
Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation Bi. Caren Rowland akiwa na waandishi wa habari leo desemba 4,2022 Jijini Dar es Salaam kukubali maoni ya YST yanayotokana na Desemba 8,2022 kwenye hoteli Serena Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment