HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 20, 2022

Kiwanda cha magari cha GF Vehicles Assemblers (GFA) chashinda tuzo ya Ubora 2022\2023 kwa makampuni makubwa nchini

 Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwan kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Ubora wa Kitaifa wa makampuni bora kwa Mwaka 2022\2023 zilizoandaliwa na shirika la viwango nchini TBS.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema wanaipokea tuzo hiyop kwa furaha kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza na kuibuka kuwa washindi wa jumla katika kipengele cha makampuni makubwa,
Pia alisema tuzo hiyo inawahasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidi Zaidi ikiwezekana mwakani washinde tuzo za kimataifa za ubora wa bidhaa na itakayoweza kuzalisha magari na kuingia katika soko la ushindani kimataifa.

Pia aliwashukuru wafanyakazi wenzake wakiongozwa na timu mzima ya wataalamu katika kutengeneza magari vitengo tofauti .

Nae mkurugenzi wa shirika la viwango nchini (TBS) Dr. Athuman Ngenya aliwataka GF kutoridhika na ushindi huo wa jumla nchini na wahakikishe wanashiriki mashindano ya nchi ya SADC katika ubora na viwango kwa makampuni ya jumuia hiyo kuibukja mshindi anapata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki mashindano ya Uboroa na viwango ya jumuia ya SADC na atakuwa anaiwakilisha Tanzania na wao kama TBS watashirikiana na GF kuhakikisha wanapeperusha vyema benderaya Tanzania.

Kwa kumalizia mkurugenzi Mtendaji wa GF Vehicles Assemblers (GFA) Imrani Karmal anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya wao kukidhi Ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi huo,Pia ameupokea ushauri wa mkurugenzi wa TBS wa lkumtaka kushiriki mashindano ya SADC ya ubora na viwango .

Akimalizia Karmali alisema kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na mahusiano mazuri na serikali Kiwanda hicho kipo katika hatua ya pili ya upanuzi ili kuweza kuzalisha magari aina zoote makubwa(truks) na madogo.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya(kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GF Vehicle Assemblers Limited,Imran Karmali tuzo ya Ubora wa Kitaifa wa Kampuni bora ya Mwaka 2022\2023  kwa makampuni makubwa wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hiyo iliyoandaliwa na TBS. jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mkuu wa GF Vehicle Assemblers, Bw. Ezra Mereng
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya(kushoto) akimkaribisha  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GF Vehicle Assemblers Limited,Imran Karmali wakati wa kupokea tuzo ya Ubora wa Kitaifa wa Kampuni bora ya Mwaka 2022\2023  kwa makampuni iliyoandaliwa na TBS  jijini Dar es Salaam . Kulia ni Meneja Mkuu wa GF Vehicle Assemblers, Bw. Ezra Mereng



 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad