HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 19, 2022

BENKI YA NMB YACHANGIA MAENDELEO YA ELIMU KIBAHA,YAMWAGA VIFYAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 37/=

 Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya kusaidia maendeleo ya elimu wilayani Kibaha vyenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 37 kama sehemu ya kuchangia ustawi wa huduma za kijamii nchini.


Kiasi hicho ni sehemu ya asilimia moja ya faida baada ya kodi ambayo benki hiyo utenga kila mwaka kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuwekezakatika miradi ya maendeleo.

Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Meneja waTawi la NMB Kibaha, Bw Festo Isango, aliyemwakilisha Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam inayojumuisha piaMkoa wa Pwani, alisema bajeti ya mwaka huu ya benki hiyo ya uwajibikaji kwa jamii ni zaidi ya TZS bilioni mbili.

“Kwa miaka kadhaa sasa, NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu (madawati na vifaa vya kuezeka), afya (vitanda, magodoro yake na vifaa vingine vya kusaidia matibabu) na kusaidia majanga yanayoipata nchi yetu,” Bw Isango alibainisha.

“Na kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tumekuwa tukitenga asilimia moja ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka,” akiongezea.

Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa ajili ya shule nne za sekondari na mbili za msingi ilifanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi Sara Msafiri, aliyeipongeza benki hiyo kwa ushiriki wake wa dhati katika maendeleo taifa.

Kwa mujibu wa Bw. Isango, kiwango cha uwekezaji cha NMB katika miradi ya maendeleo ni kikubwa sana kinachoifanya benki hiyo kuwa kinara wa ustawi wa jamii miongoni mwa taasisi za fedha nchini na vifaa waliyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wao katika maendeleo ya jamii.

Shule zilizopata msaada wa benki hiyo jana ni shule za msingi Sofu na Mwanabwito. Za sekondari ni Mwanalugali, Pangani, Kibaha Girls na Mbawa Miswe. Usaidizi zilizoupata ni wa samani za ofisi za walimu, meza na viti vya wanafunzi, vitanda, makabati pamoja na mabati.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Sara Msafiri, akiangalia kabati za kuhifadhia vitabuzilizotolewa kwa Shule ya Msingi Sofu sh. Milioni 37 iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kibaha, Festo Issango
 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Sara Msafiri, akiangalia Viti 50 na meza vilitolewa katika hafla ya makabidhiano ya misaada mbalimbali kutoka NMB kwa shule sita wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 37 kwaShule ya Sekondari Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa shule za Sekondari na msingi za wilayani Kibaha mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad