HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 19, 2022

WATUMISHI TIRA WATAKIWA KUWAELIMISHA WANANCHI UMUHIMU WA BIMA KWA LUGHA RAHISI

  
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akizunngumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) uliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Desemba 19, 2022 jijini Tanga.
 
 =======   ======   =======
 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wametakiwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kwa lugha rahisi ili kuwezesha jamii kufahamu zaidi umuhimu wa bima hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) uliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Desemba 19, 2022 jijini Tanga,  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa ni wajibu sasa wa watumishi wa bima kuwa wabunifu katika utoaji wa elimu ili kuhamasisha watu wengi wanajiunga ili kusaidia jamii lakini pia kuongeza mapato ya nchi.

''Niwakati sasa kufikiria kuendesha kazi zenu kidigitali ili kuwezesha mambo mengi zaidi kwenda kwa urahisi, kwani Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nia yake kubwa ni kuona taasisi nyingi za kiserikali zikitekeleza majukumu yao kidigitali zaidi'' Alisema Dkt. Ndumbaro.

Aidha Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi kuweka usiri zaidi katika kutoa huduma ili kuwepo usiri baina na mtumishi na mteja Sambamba na kuzingatia uzalendo na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Kwa upande wake Kamishina wa Bima Tanzania, Baghayo Saqware amebainisha changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwenye sekta ya bima ambayo ni kutokuwepo kwa sera ya bima hapa nchini pamoja na kutokuwepo kwa bodi ya taifa ya bima na hivyo kupelekea mambo mengi ya kiutumishi kukwama.
Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware akizunngumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) uliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Desemba 19, 2022 jijini Tanga.
Naibu Kamishna wa Bima Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said akizunngumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) uliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Desemba 19, 2022 jijini Tanga.
Baadhi ya Wafanyakakazi wa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wakiwa kwenye Mkutano huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad