HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 2, 2022

TAKUKURU TANGA YABAINI USAJILI WA WAGONJWA HEWA WA VVU KWENYE MIFUMO YA USAJILI WA WAGONJWA VITUO VYA AFYA

 

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Zainabu Bakari akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022.

NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Tanga(Takukuru) imefanikiwa kudhibiti wagonjwa hewa 313 wa VVU kwenye mfumo wa usajili wa wagonjwa hao wilayani Muheza.

Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Zainabu Bakari akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022.


Ambapo alisema Takukuru kupitia vyanzo vya siri ilibaini kuwa watoa huduma za afya wanaohusika na kusajiliwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,wamekuwa wakifanya udanganyifu kwa kuwaingiza majina hewa ili kuonesha takwimu za wanaoishi na VVU kuonekana zipo juu kwa maslahi yao binafsi.


Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Tanga alisema alisema katika ufuatiliaji wa Takukuru Mkoa ulibaini kuwa wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kuwasajili na kuwafuatilia wagonjwa wanaoishi na VVU wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri ka mawasiliano kiasi cha sh 20,000 kwa siku kila wanapotoka kwenda kukutembelea wagonjwa hao.


Alisema kwamba fedha hizo kulipwa na Shirika la Afya la Amref kwa kazi ya kufuatilia kila mgonjwa kwa lengo la kuhakikisha hali yake kiafya inaimarika kwa maana ya kutumia dawa kwa wakati na huduma nyengine zinazostahili.


Aidha alisema fedha hizo kulipwa moja kwa moja kwa mhudumu husika kupitia namba yake ya simu ya mkononi na ndiyo sababu inavyopelekea watumishi wasio waadilifu kuweka takwimu hewa kwa lengo la kujiongezea posho.


Alieleza katika ufuatiliaji uliofanywa na Takukuru kwa baadhi ya Zahanati ilibainika kuwa ni kweli kuna wagonjwa ambao hiyo halisi kwa maana ya upatikanaji wake na hivyo kufanya udhibiti kwa kuchukua hatua.


Alisema kwamba hatua walizoanza kuchukua ni kufikisha kikao cha pamoja kati yao na ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya na watendaji wake wote wanaohusika na kuwahudumia watu wanaoishi na VVU pamoja na Amref.


" Katika kikao Takukuru iliwasilisha yaliyobainika katika ukaguzi wa kutembelea Jumla ya zahanatini 7 kati ya 16 zilizopo katika wilaya ya Muheza na kubaini tatizo hilo"Alisema.


Hata hivyo alisema kwamba katika kikao kazi hicho taasisi hiyo mkoani hapa ilimuagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza kufanya uhakiki wa takwimu za wagonjwa wote wanaoishi na VVU na kutoa taarifa ya uhakiki.


Alisema baada ya agizo hilo ilibainika kuwepo kwa Jumla ya wagonjwa hewa 313 ambapo idadi hiyo iliondolewa kwenye mfumo.


Pia alisema wahusika katika usajili wa wagonjwa hao hewa wamepewa barua za kujitoleza kwa kitendo cha usajili wagonjwa hewa huku Wizara ya Afua ikitoa maelekezo ya kufanyika uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambao sio halisi.


Hata hivyo Taasisi hiyo inaendelea kuwasihi watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa mujibu wa kanuni,taratibu,sheria na kiongozi iliyopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad