HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 2, 2022

MFUMO WA e-GAZETI YAZINDULIWA KWENYE MY VODACOM APP

Wapili kulia ni Meneja Uhusiano wa Kibiashara na Masoko wa Mwananchi Communications Ltd,  Vivian Temi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022. Kutoka Kushoto ni Meneja umiliki wa bidhaa kutka Vodacom, Sarah Athanas, Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa Vodacom, Nguvu Kamando na wa Kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kiigitali w Mwananchi Communicatins Ltd, Sebastian Nkoha. 

Meneja Uhusiano wa Kibiashara na Masoko wa Mwananchi Communications Ltd,  Vivian Temi, Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa Vodacom, Nguvu Kamando wakikata utepe kuashilia Uzinduzi wa Mfumo wa e-Gazeti ndani ya My Vodacom App jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022.

Meneja Uhusiano wa Kibiashara na Masoko wa Mwananchi Communications Ltd,  Vivian Temi na  Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa Vodacom, Nguvu Kamando wakionesha mfano wa aplikesheni ya e-Gazeti itavyokuwa inaonekana kwenyesimu.
 Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa Vodacom, Nguvu Kamando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022 wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa e-Gazeti ndani ya My Vodacom App kulia ni Meneja Uhusiano wa Kibiashara na Masoko wa Mwananchi Communications Ltd,  Vivian Temi akionesha namna Aplikesheni ya e-Gazeti itavyokuwa inasomeka kwenye kishikwambi, Simu na Laptop.
Picha na Avila Kakingo, Michuzi tv

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania wakishirikiana na Mwananchi Communications LTD wameendelea kukuza Mageuzi ya Kidigitali nchini kupitia bunifu na Uwekezaji nchini kwa kukuza usomaji wa magazeti Kidijitali Kupitia programu ya e-Gazeti kwenye Aplikesheni ya My Vodacom App.

Meneja Uhusiano wa Kibiashara na Masoko wa Mwananchi Communications Ltd,  Vivian Temi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 2, 2022 wakati wa Uzinduzi wa e-Gazeti ndani ya My Vodacom App amesema kuwa Aplikesheni hiyo itawawezesha wateja wa Vodacom kuelimishwa na kuhabarishwa kupitia nakala magazeti ya Mwananchi Comminications Ltd.

Amesema kuwa waliona kunafursa ya kuwafikia watanzania wengi zaidi na magazeti ya Kidigitali kwa kushirikiana na Vodacom kwani ni mtandao unaopatikana kote nchini.

"Kupitia utandawazi kunaurahisi wa kuwafikishia watanzania wengi zaidi, Magazeti kidigitali na sasa kupitia aplikesheni ya My Vodacom App tunawaletea wateja wa Vodacom huduma yetu ya e-Gazeti kwa ukaribu zaidi lengo likiwa ni kufungua fursa, kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha. Amesema Vivian

Ameongeza kuwa kupitia My Vodacom App wateja wanaweza kusoma magazeti ya MCL kwa Urahisi na kwa gharama nafuu, pia wataweza kupata nakala hizo mapema saa sita usiku. Na kupitia e-Gazeti wateja wanaweza kutunza kumbukumbu za Magazeti kwa kupitia Maktaba inayopatikana kwenye huduma ya e-Gazeti.

"Vodacom wamekuwa wadau wetu wakubwa katika kutimiza malengo yetu kama kampuni kwa kuwahabarisha watanzania na kuzua mijadala yenye manufaa kwa taifa letu na ndio maana tunaendelea Ubia huu. Kupitia e-Gazeti tunatarajia kufikia watu laki mbili na tunategemea waliowengi kunufaika na urahisi wa kupata magazeti yetu ya Mwananchi, Mwanaspoti, Citizen na Jarida la Mwananchi Scoop." Amesema Vivian

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa Vodacom, Nguvu Kamando amesema kuwa Kampuni Vodacom ina dira ya kuipeleka Tanzania kwenye Ulimwengu wa Kidigitali na kuboresha maisha ya watanzania kupitia Teknolojia, kutanua umhimu wa habari katika maendeleo ya taifa ndio maana wamewaunga mkono MCL ili kupanua wigo wa Kusambaza magazeti kwa watanzania zaidi ya Milioni 17 wanaotumia Mtandao wa Vodacom.

"Maisha ya Watanzania wengi ni ya Kidigitali kuanzia kufanya manunuzi na Malipo, kupata burudani, Usafiri, kujielimisha na kupata habari, ndio maana tunaendelea kupanua wigo wa aplikesheni ya My Vodacom App ili wateja waweze kupata huduma nyingi zaidi kwenye aplikesheni ya Vodacom." Amesema Nguvu

Uzinduzi huo unaenda sambamba na Kampeni ya "Habari Ziendelee." inayoendeshwa na MCL ikiwa na lengo la kuhamasisha usomaji wa magazeti Kidigitali kupitia Simu Janja, Laptop pamoja na Vishikwambi.

Ili kupata huduma hiyo Wateja wa Vodacom watatakiwa kupakua App ya My Vodacom kupakua Aplikesheni ya My Vodacom inayopatikana kwenye play store kwa watumiaji wa Android au App store kwa watumiaji wa IOS. Kisha watabofya. kwenye huduma za Kidijitali baada ya hapo chini kabisa utaona alama ya e-Gazeti 

Bofya kisha subscribe na uanze kusoma na kufurahia Magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen na Jarida la Mwananchi Scoop. Gharama za gazeti ni Shilingi mia tano kwa magazeti yote matatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad