Na Mwandishi Wetu, Geita
TIMU
ya watoto ya Mgusu Machinjioni imefanikiwa kutwaa taji la GGML- Toto
Cup baada ya kuifunga timu ya Elimu Uwangani kwa jumla ya mabao 2-0
katika mchezo wa fainali uliofanyika Nyakabale wilayani Geita mkoani
Geita.
Mgusu Machinioni
walitangazwa kuwa mabingwa wa mashindano hayo ya soka ya watoto
yanayofanyika kwa kushirikisha watoto wanaozunguka migodi wa Kampuni ya
Geita Gold Mining Ltd. (GGML)
GGML
ambao ndio waanzilishi na waandaaji wa mashindano hayo, walizindua
michuano hiyo katika kata za Mtakuja na Nyankumbu za Geita Mjini kwa
lengo la kutoa elimu kwa watoto, walezi na wazazi kuhusu madhara ya
kuwanyonya watoto wadogo katika shughuli za uchimbaji madini na
kuwanyima fursa ya masomo.
Akizungumza
katika fainali hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong alielezea furaha yake kwa
kuhudhuria katika kilele cha mashindano hayo ya kandanda kwa vijana
kutoka eneo jirani la mgodi.
Alibainisha
kuwa tangu kuanza kwa shughuli zao mkoani Geita, uvamizi wa watoto
wadogo umekuwa ni changamoto kubwa kwenye eneo la mgodi.
Hata
hivyo, alisisitiza kuwa watoto ni sehemu muhimu ya jamii inayozunguka
mgodi huo katika kutekeleza shughuli zao za kibiashara.
"Kama
sehemu ya kujitolea kwetu kwa jamii, tumefanya uwekezaji mkubwa katika
shule, hospitali na kuchangia vifaa mbalimbali vya kutoa huduma.
Mathalani mwaka 2018, GGML ilijenga zaidi ya madarasa 600.
“Hii
yote ni katika kuwajengea mazingira mazuri ya elimu kwa watoto wetu
kwani watoto ni kizazi cha siku zijazo na ndio wanufaika wa kwanza
jitihada zote tunazozifanya katika kujitolea kwetu,” alisema Strong.
Alibainisha
kuwa kampuni hiyo inazingatia Kanuni Elekezi za Umoja wa Mataifa kuhusu
Biashara na Haki za Kibinadamu na Kanuni za Hiari za Usalama na Haki za
Kibinadamu (VPSHR) (UNGP).
"Kwa hivyo, tumeahidi kuwalinda watoto dhidi ya hatari zozote zinazohusiana na mazoea yetu ya biashara," alisema.
Aidha,
kwa mujibu wa Strong, idadi ya watoto wanaovamia na kuingia kwenye eneo
la mgodi ni jambo ambalo linachukuwa kwa tahadhari kubwa na mgodi huo.
"Kwa
kawaida sisi hutumia neno "kuwaokoa watoto" badala ya "wavamizi" kwa
sababu watoto wanalindwa na sheria za kitaifa na kimataifa. Hata hivyo,
imefahamika kwamba idadi kubwa ya watoto waliookolewa katika eneo la
mgodi wanapatikana ndani au nje ya eneo la mgodi wetu,” alisema.
Alisema kati ya mwaka 2019 na 2020, watoto 680 waliokolewa ndani na nje ya eneo la uendeshaji la GGML.
Alisema
ili kukabiliana na hali hiyo, GGML imeshirikiana na serikali za mitaa
kuanzisha programu kadhaa za uhamasishaji, ikiwa ni pamoja na
mawasiliano ya moja kwa moja na shule za sekondari na msingi.
Strong
alisema, "Katika jitihada za kuwaweka watotokuwa wachangamfu, washiriki
program mbalimbali wakati wa mapumziko ya likizo na kukuza hamasa ya
kuwa na afya njema, tumechagua kufadhili mashindano ya kandanda kwa
ajili ya vijana waliopo ndani na nje ya eneo la mgodi."
“Tunaamini
kuwa kila shindano linapohitimishwa, wachezaji wenye vipaji vya soka
wataibuka na kuchaguliwa na klabu kubwa kama Geita Gold Football Club
(inayodhaminiwa na GGML) kuchuana katika uwanja wa Magogo ambao pia
unadhaminiwa na GGML, lengo ni kuwaokoa hawa na kuwasaidia kukuza vipaji
vyao kisoka,” alisema.
No comments:
Post a Comment