HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 9, 2022

TAARIFA YA POLISI KUHUSU AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI MKOANI MBEYA

 


Mnamo tarehe 09.11.2022 majira ya saa 12:45 asubuhi huko eneo la Mlima Iwambi nje kidogo ya Jiji la Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma, Gari Basi yenye namba za usajili T.601 DXC aina ya Fuso linalofanya safari zake kati ya Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga likitokea Mbeya liligonga Gari namba T.452 DHD aina ya Toyota Raum na kusababisha vifo vya watu wawili watoto waliokuwa kwenye Gari ndogo namba T.452 DHD aina ya Toyota Raum na majeruhi kwa watu watatu kati yao mwanaume mmoja na wanawake wawili.


Aidha Gari hilo T.601 DXC Fuso Basi liliendelea kugonga Gari jingine lenye namba za usajili T.673 DMV lenye Tela namba T.362 DMG aina ya Scania lililokuwa linaelekea Mbeya na Gari namba DAD 3981 na Tela lake ABF 75591 aina ya Dofeng lililokuwa limebeba madini aina ya Sulpha.


Chanzo cha ajali ni mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali. Jitihada za kumtafuta Dereva zinaendelea. Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mbeya.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga anatoa wito kwa madereva kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa madereva kufuata utaratibu uliowekwa wa kupitisha magari ya abiria na malori kwa muda tofauti katika maeneo yenye milima na miteremko mikali ili kuepuka ajali na madhara makubwa yasitoe kwa abiria.


Imetolewa na,

ACP – Benjamin E. Kuzaga

Kamanda wa Polisi,

MKOA WA MBEYA.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad