HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 28, 2022

MOROCCO ILEEEE…KOMBE LA DUNIA

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya taifa ya Morocco imeendelea kuchanja mbuga katika Michuano ya Kombe la Dunia, 2022 nchini Qatar baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ngumu ulimwenguni ya Ubelgiji ikiwa ni mchezo wa Kundi F la Michuano hiyo.

Mabao ya Morocco katika mchezo huo yamefungwa na Kiungo Mshambuliaji wa timu hiyo, Abdelhamid Sabiri dakika ya 73’ na bao la pili limefungwa na Mshambuliaji, Zakaria Aboukhlal.

Morocco wakiwa wanakilisha bara la Afrika katika Michuano hiyo, hadi sasa wana alama nne wakiwa wanaongoza Kundi hilo la F, huku wakiwa na alama tatu, Croatia alama moja sawa na Canada wenye alama hiyo moja pekee.

Mchezo wa mzunguko wa mwisho Morocco watacheza dhidi ya Canada huku Ubelgiji watakabiliana na Croatia ili kupata timu mbili zitakazofuzu hatua ya 16 ya Michuano hiyo inayoendelea nchini Qatar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad