HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 28, 2022

SIMBA SC YAIPIGISHA KWATA POLISI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
SIMBA SC imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC Premier League) katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi na kufikisha alama 32 katika msimamo.

Katika mchezo huo, Wekundu wa Msimbazi wamepata mabao yao kupitia Mshambuliaji John Raphael Bocco dakika ya 32’ na mabao mawili yamefungwa na Mshambuliaji Moses Phiri dakika ya 43’ na 53’.

Baada ya kipigo hicho kutoka kwa Simba SC, Kocha wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema Wachezaji wake walianza vizuri mchezo huo, lakini baadae walipoteza umakini (Concentration) na kupelekea kufungwa mabao matatu, hata hivyo amesema watafanya usajili katika baadhi ya maeneo ili kuboresha Kikosi chao.

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema mchezo unaofuata wanaenda kuwakabili Coastal Union FC ya Tanga katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mgunda amesema: “Coastal Union tunawajua vizuri wakiwa nyumbani, lakini tutajipanga kucheza nao katika mchezo huo unaofuata”.

Kocha Mgunda amemzungumzia Kiungo Clatous Chama, amesema Chama ana kiwango kizuri sanjari kushirikiana na wenzake katika kutekeleza majukumu ya timu pindi iwapo uwanjani katika michezo mbalimbali.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad