MAFUNZO UTUNZAJI TAARIFA BINAFSI MTANDAONI YATOLEWA KWA WALIMU, WANAFUNZI,VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 28, 2022

MAFUNZO UTUNZAJI TAARIFA BINAFSI MTANDAONI YATOLEWA KWA WALIMU, WANAFUNZI,VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA

 

NA Said Mwishehe, Michuzi TV

ASASI ya  AGENDA imeshauri kwamba umefika wakati kwa sasa kufanyika utafiti kwa ajili ya kuangalia madini ya risasi yanayotumika kwenye utengenezaji wa rangi ili kuwa na uhakika ikiwa nchi yetu haizalishi tena, kusambaza, kuuza au kutumia rangi zenye risasi.

Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 27,2022 jijini Dar es na Asasi ya AGENDA wakati wa maadhimisho ya Wiki ya kimataifa ya kuzuia madhara ya madini ya risasi na dhamira kuu ni kulinda afya ya watoto kwa kuongeza kasi ya utekelezaji hatua za kuondoa matumizi ya rangi zenye madini ya risasi.

 “Tangu mwaka 2009 , asasi na mashirika wanachama wa IPEN zimefanya tafiti zaidi ya 100 kwenye rangi zaidi ya 4,000 kutoka nchi 59 ikiwemo Tanzania ambako AGENDA ilishiriki , na utafiti wa mwisho ulifanywa na GENDA mwaka 2017 ambapo asilimia 46 ya rangi za mafuta zinazotumika kupamba majengo na vitu  vinavyotumia na zinazouzwa nchini Tanzania zilionekana kuwa na kiwango cha risasi zaidi ya sehemu 90 kwa mamilioni baadhi zikiwa na kiwango cha juu sana vya risasi hadi sehemu 84,000 kwa milioni,”amesema.

Hivyo amesema kwa sasa kuna haja ya kufanya utafiti sawa na huo ili kuwa na uhakika ikiwa nchi ya Tanzania haizalishi tena, kusambaza, kuuza na kutumia rangi zenye risasi  huku akieleza ushahidi wa miongo kadhaa umeonesha kuwa hakuna kiwango salama cha madini ya risasi.

“Risasi ni sumu kali inayoathiri mifumo mingi ya mwili nan i hatari sana kwa watoto wadogo walio chini ya miaka sita, Hata katika kipimo cha chini , risasi inaweza kuathiri ukuaji wa ubongo na watoto na hivyo kusababisha kupungua kwa kiwango cha uelewa au uakili(IQ)…

“Mabadiliko ya kitabia kama vile kupungua figo, viungo vya uzazi na mifumo wa kinga na kusababisha upungufu wa damu na shinikizo la damu.Athari katika mfumo wa fahamu na za kitabia zinazosababishwa na risasi kwa kawaida haziwezi kutenduliwa au kuondolewa,”amesema.

Kwa upande wake Ofisa Programu Mkuu wa AGENDA Silvani Mng’anya amesema ili kukomesha matumizi ya rangi zenye risasi nchini Tanzania , AGENDA inatoa mwito kwa Serikali ikijumuisha Shirika la Viwango Tanzania(TBS), ofisi ya makamu wa Rais –Idara ya mazingira , Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Mazingira la Usimamizi wa Mazingira(NEMC),Mamlaka ya Usalama wa Afya Mahali pa Kazi(OSHA) na wadau wengine kutekelez kwa uthabiti kiwango cha udhibiti wa risasi katika rangi ambacho kilipitishwa mwaka 2017.

Aidha watengenezaji wa rangi, waagizaji, wasambazaji  na wauzaji waunge mkono juhudi za Serikali kwa kushughulika na rangi isiyo na risasi pekee .Hilo linawezekana kabisa na tayari baadhi ya watengenezaji wa rangi wamekuwa wakitengeneza rangi isiyo na risasi  kwa zaidi ya mitano sasa.

“Serikali na wadau wengine kutoa elimu ya uelewa kwa umma kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya rangi zenye risasi.Pia wanatoa mwito kufanyika utafiti mpya ili kujua hali ya sasa kwa rangi nchini Tanzania, miaka mitano baada ya kiwango cha kitaifa kuidhinishwa,”amesema.

Pamoja na hayo amesema AGENDA ni asasi isiyo ya kiseikali inayokusudia kukuza utamaduni wa kuwajibika kwa mazingira miongoni mwa umma kwa ujumla kupitia uhamasishaji , utetezi , kujenga uwezo na ushiriki wa wadau nchini Tanzania na kwingineko.

Aidha amesema katika Wiki ya kuongeza uelewa duniani, AGENDA imefanya mkutano na wadau ili kushirikishana jitihada zinazochukuliwa katika kutekeleza kiwango cha Taifa cha rangi kilichopitishwa na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) mwaka 2017 cha sehemu 90 milioni(milioni 90)kama kiwango cha juu cha risasi katika rangi .Pia inashiriki kutoa habari kwa umma ili kuwafahamisha kuhusu wiki hii muhimu na juhudi ambazp nchi imezifanya katika kuondoa madini ya risasi katika rangi nchini Tanzania.

“AGENDA ni mwanachama wa Mtandao wa Kimataifa wa kutokomeza uchafuzi –International Pollutants Elimination Network(IPEN) unaojumuisha asasi na mashirika ya kutetea watu kutoka nchi  125 duniani kote katika kuondoa kemikali , taka na vichafuzi vya sumu.IPEN ni mwanachama mwanzilishi wa muungano wa kimataifa wa kuondoa risasi katika rangi.”amesema Mng’anya.

Wakati huo huo Ofisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kuruthum Nancy Shushu amesema wao majukumu yao makubwa katika kupunguza madini ya risasi ni pamoja na kuhakikisha maeneo ambayo yanahusika na bidhaa zinazotumia madini hayo ya risasi kwa mfano viwanda vya rangi wanahakikisha viwanda hivyo vinazingatia matakwa ya sheria ya mazingira.

“Miongoni mwa matakwa ya Sheria ya Mazingira ni kuhakikisha viwanda vinakuwa na vyeti vya tathimini ya mazingira ambavyo wamevipata baada ya Baraza kujiridhisha kuwa upo usalama wa kutosha wa kuzuia wafanyakazi kutoathrika na madini hayo wanapokuwa sehemu za kazi kwa maana ya viwandani.Lakini kwa upende mwingine baaza linatoa vibali vya kujishughulisha na taka hatarishi mbalimbali ikiwemo betri na taka nyingine ambazo tunaamini mara nyingi zinakuwa zimetengenezwa sana na madini ya risasi.

“Na bidhaa hizo zikashakuwa taka zinahitaji utaratibu maalumu wa kuharibiwa , kuteketezwa au kurejerezwa kwa maana tuna viwanda vya kurejezwa betri chakavu kwa hiyo viwanda hivyo tunahakikisha pia vinapokea betri kwa watu ambao wamesajiliwa na Baraza  kwa ajili ya kukusanya, kusafirisha betri chakavu au taka ngumu zote ambazo tunaamini zinamadini ya risasi ili kuhakikisha madini hayo hayawezi kutoka au kuharibu mazingira na kuifikia jamii,”amesema Shushu.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa ASASI ya AGENDA Haji Rehani amesema kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuondoa madini ya risasi ambapo amefafanua mwanzoni Tanzania iliungana na dunia katika kuondoa madini ya risasi kwenye mafuta ya petroli na ikafanikiwa na sasa wako kwenye kuangalia changamoto nyingine ambazo zinachangia uchafuzi wa mazingira na mojawapo ni matumizi ya rangi yaliyoongezewa madini ya risasi wakati wa uaandaji wake.

“Kwa hiyo tunaungana na dunia katika mchakato wa kuondoa uchafuzi wa madini ya risasi kwenye mazingira hasa ambayo yanakuwa mazingira ya nyumbani zaidi, kama unatumia nyumbani na watoto wanaila wanapata athari kwa urahisi na unakuta changamoto kubwa kwa rangi ambazo zimeshaanza kuharibika inakawaida ya kutoa rangi na kudondosha vumbi na madini yale huwa yanaladha kama ya sukari na watoto wanapenda kulamba , kwa hiyo inakuwa rahisi kuathirika zaidi.” MAOFISA wa Asasi ya AGENDA wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali kutoka taasisi za umma baada ya kumalizika kwa majadiliano yaliyohusu kuangalia ni namna gani Watanzania wanaweza kushiriki kikamilifu katika kuzuia madhara ya madini ya risasi ikiwa ni mpango mkakati wa kidunia wa kuondoa madhara ya madini hayo hasa kwa watoto.Aidha AGENDA imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha wiki ya kuzuia madini ya risasi.Ofisa Programu Mkuu wa AGENDA Silvani Mng’anya (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa Wiki ya Kimataifa ya Kuzuia Madhara ya Madini ya Risasi kwenye rangi.Katikati ni Ofisa Programu Mwandamizi wa asasi hiyo Dorah Swain na kulia ni Katibu Mtendaji Hani Rehani.

Viwango kutoka Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Joseph Nziku (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa majadiliano hayo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad