Na Mwandishi Wetu, Ufaransa
KUTOKANA na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, bidhaa nyingi na zenye ubora kutoka Tanzania zimeanza kupata masoko katika nchi za Ulaya.
Hayo ni maparachichi kutoka Tanzania ambayo yanauzwa katika "supermarket" kubwa iitwayo Carrefour mjini Paris, Ufaransa. Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa unatoa mwito kwa wakulima na wafanyabiashara nchini Tanzania waandelee kuzalisha kwa wingi bidhaa zenye ubora kwa ajili ya masoko ya nchi za Ufaransa, Uhispania na Ureno.
Kwa mujibu wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa umeeleza kwamba "Tunawaomba wakulima na wafanyabiashara wa aina mbalimbali kuzalisha kwa wingi bidha nyingi na zenye ubora, soko katika nchi za Ulaya ni kubwa, hivyo ni wakati wetu kutumia soko hilo kuuza bidhaa za kutoka nyumbani."ni
No comments:
Post a Comment