HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 7, 2022

TIGO YASHIRIKIANA, BOOMPLAY KUIMARISHA USIKILIZAJI WA MUZIKI KIDIJITALI TANZANIA

 


 
Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za mawasiliano nchini Tanzania, Tigo, leo Septemba 7,2022  imetia saini na kutangaza ushirikiano wa kimkakati na App namba moja barani Afrika, Boomplay, utakaowawezesha wateja wa Tigo kupata unafuu wa gharama na kusikiliza muziki bure kupitia App ya Boomplay kama sehemu ya Kampeni ya Wakishua.

Kampeni ya Wakishua inadhihirisha dhamira ya Tigo katika kuboresha mageuzi ya kidijitali kwa wateja kote nchini huku ikitafakari kuhusu mabadiliko ya chapa kwa wakati.Wateja wa Tigo nchini Tanzania kuanzia sasa, mara baada ya kujiunga na vifurushi vya siku, wiki au mwezi watasikiliza muziki bure kupitia App ya Boomplay.

Sambamba na hilo, wateja wa Tigo watafurahia punguzo la asilimia 30 watakapohitaji kujiunga na malipo ya  siku, wiki au mwezi ya Boomplay.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tigo, William Mpinga alisema, "Mtandao wa Tigo umekuwa ukisaidia tasnia ya muziki kwa muda sasa kwa kutoa fursa kwa wasanii kuungana na mashabiki zao, hivyo tuna furaha kutoa jukwaa litakalo endeleza dhumuni hili.

Amesema wanatambua  hitaji la wateja nchini Tanzania kuwa na chaguzi zaidi za kupata muziki na burudani, na kukidhi hitaji hili; hakuna mtoa huduma bora wa kushirikiana nae zaidi ya Boomplay.

Ameongeza  kupitia uzinduzi wa kampeni hii ya Wakishua, tunawapa wateja wetu jukwaa la kidijitali ili kusikiliza bila malipo, ubora wa sauti na machaguo mapya ya muziki.

Pia akizungumzia ushirikiano huo, Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli, alisema, "Maono yetu ni kuwezesha sekta ya muziki wa Kiafrika na kuhakikisha unafika mahala pazuri, hivyo, tuna matumaini makubwa kupitia ushirikiano huu na Tigo.

"Tunaamini ushirikiano wetu utaongeza usikilizwaji wa nyimbo zaidi ya milioni 85 kwenye App ya Boomplay na kuongeza kipato kwa wasanii wa Tanzania katika siku za usoni”.


Ameeleza Kampeni ya Wakishua inaruhusu wapenzi wa muziki kuwasikiliza wasanii wanaowapenda wa ndani na nje ya Tanzania kwa kutumia fursa ya ofa ya usikilizaji muziki bila malipo kupitia Boomplay na hatimaye kuongeza kipato kwa wasanii hao.

Ameongeza kuwa Wateja sasa wanaweza kufurahia machaguo mbalimbali ya muziki kwenye App ya Boomplay kwa kununua kifurushi chochote kutoka Tigo. Kwa wale ambao bado hawapo kwenye mtandao wa Tigo, wanaweza kupata SIM kadi ya Tigo kote nchini na kupakua App ya Boomplay na kuwa sehemu ya kundi la Wakishua.

Pia Watumiaji wa Boomplay kupitia mtandao wa tigo wanahimizwa kusasisha programu yao ya Boomplay hadi toleo jipya zaidi ili kufurahia vipengele na matoleo mapya. Ofa ya Wakishua inapatikana tu kwenye toleo la programu ya Boomplay v6.1.20 na matoleo mapya zaidi kwenye Android na v4.4.0 na matoleo mapya zaidi kwenye iOS.

Kuhusu BoomplayBoomplay ni App inayoongoza kwa utoaji huduma ya kupakua na kusikiliza muziki barani Afrika. App ya Boomplay inajumuisha mamilioni ya nyimbo, video na habari za burudani ambazo huwawezesha watumiaji wake kusikiliza na kupakua nyimbo na video wanazozipenda na kujiunga na huduma za kipekee kama vile kusikiliza muziki bila matangazo na kuhifadhi muziki kwa ajili ya kusikiliza bila bando.

Hivi sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji milioni 70 wa kila mwezi (MAU) na idadi ya nyimbo zaidi ya milioni 80.Huduma hii inapatikana duniani kote kwenye simu kupitia Google Play Store ya Android, App Store ya iOS na kwenye tovuti kupitia www.boomplay.com. Kampuni hiyo ina ofisi za kanda nchini Tanzania, Nigeria, Ghana, Kenya, Cote d'Ivoire na Cameroon.

Kuhusu TigoTigo ilianzishwa mwaka 1994 ikiwa mtandao wa kwanza Tanzania wa simu za mkononi. Ni kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu mkubwa nchini na ambayo inatoa huduma zinazolenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika maisha ya watanzania.

 Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music (Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husikaTigo ni sehemu ya Axian Telecom.

AXIAN Telecom ni Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Ki-afrika inayotoa huduma katika nchi nane kupitia kwenye matawi yake ya Madagascar, Comoros, Reuniuon, Mayotte, Senegal, Togo, Uganda na Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad