HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 7, 2022

RC MGUMBA AUPONGEZA MFUKO WA SELF MICROFINANCE KWA KUKUZA MTAJI WAKE

Na Mwandishi Wetu,Tanga.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameupongeza Mfuko wa Self Microfinance kwa kuweza kukuza mitaji yao kutoka Bilioni 57 mwaka June 2016 hadi kufikia Bilioni 59.8 June 2022 jambo ambalo ni muhimu kwa ustawi wake.

Mgumba aliyasema hayo wakati akifungua matawi manne ya Mfuko huo yaliyopo mkoani Tanga, ambapo alisema zipo taasisi nyingi zimepewa mbegu na Serikali lakini imekufa maana yake walikula lakini nyie ni taasisi inayofaa zaidi na kuungwa mkono kwa kuweka mbegu zaidi kwa sababu mtaji upo salama na inaendelea kukua siku hadi siku.
Mkuu huyo alisema amefarijika zaidi kwa  mpango mkakati wa kuhakikisha wanaongeza matawi ili kufika mikoa yote na atafarijika kuona Mfuko huo unatekezwa n kufanya kazi Tanzania bara  na Visiwani.

Alisema, Serikali inafahamu Mfuko wa Self Microfinance ni moja ya taasisi muhimu ya fedha katika ustawi wa maendeleo ya uchumi katika  nchi.

"Nimesikia katia kipindi cha miezi sita mmetoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 16.4 kwa wakopaji 3019 na kwamba mmeanzisha huduma za mikopo kwa wajasiriamali  wadogo na wakati, mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali na watumishi wa umma ni jambo jema ni nyie ni taasisi mliomuelewa Rais Samia Suluhu katika kuwahudumia watanzania hususani wenye kipato kidogo na wenye mazingira magumu ya kufikia mitaji na mikopo kwenye taasisi za fedha"Alisema.
kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo, Paul Sangawe alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu kwa imani kubwa ambayo  aliionyesha kwao kuweza kuwakabidhi jukumu hilo la kusimamia utekelezaji wa taasisi hiyo, huku akiahidi kufafanya kazi kwa bidii na kwa uwezo wao wote kuhakikisha kwamba kazi na tija ya utekelezaji wa jukumu ya Mfuko inaongezeka.

Alisema ni matumaini yake kwamba ushirikiano huo utaendelea ili kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kuweza kutimiza malengo ya Mfuko huo huku akieleza mafanikio hayo yanatokana wajumbe wa bodi.

Alisema pia waliandaa mpango mkakati wa Mfuko kwa kuhakikisha wanapanua  mtandao wa huduma kutoka matawi 4 hadi 12 na hivyo kuweza kufikia wateja kwa haraka zaidi ikiwemo kuongeza  huduma za mikopo kwa walengwa wa mfuko  kutoka 7 hadi 10 hivyo wananchi wameweza kuchagia hivyo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Mudith Cheyo alisema wajasiriamali wapatao 191,865 nchini wamenufaika na mikopo kutoka Mfuko wa Self Microfinance  yenye thamani ya Bilioni 242 hadi kufikia June 2022 na hivyo kusaidia kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kukuza mitaji yao.

Alisema utoaji wa mikopo hiyo ulikwenda sambamba na utoaji wa mikopo kwenye taasisi ndogo za kifedha, Pia kuanzisha huduma za mikopo ya moja kwa moja kwa muhusika ambapo ilikuwa ikiwalenga wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs), mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo na mikopo kwa watumishi wa umma .
Aidha alisema utoaji wa aina hiyo ya mikopo ni mageuzi makubwa katika kumuinua mtanzania wa kawaida kimapato na kukuza ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa Taifa.

"Tunajivunia kuwa na bodi mahiri ya wakurugenzi ya Mfuko wa Self kwani chini ya usimamizi wao tumepata mafanikio mengi na ya kutia moto kwani hata idadi ya wafanyakazi imeongezeka kutoka 30 mwaka 2015 hadi 70 Sasa lakini mtandao wa matawi nao imeongezeka kufikia 12"Alisema Afisa Afisa Mtendaji huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad