TLB WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWASHIRIKISHA KUTOA MAONI YA SENSA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 13, 2022

TLB WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWASHIRIKISHA KUTOA MAONI YA SENSA

Wanachama wa chama cha wasiiona Tanzania na Swedeni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya majadiliano wa Namna ya kuwaendeleza watu wasioona hapa nchini. 


Meneja wa Mradi wa Mradi wa kudahili watoto wenye ualbino na wasioona wa Haki Yangu (MY RIGHT SRF, kutoka Sweden Eva Nilsson akizungumza watu wasioona wa Wilaya ya Kinondoni pale walipofika na kuzungmza nao.
Meneja wa Mradi wa Mradi wa kudahili watoto wenye ualbino na wasioona wa Haki Yangu (MY RIGHT SRF, kutoka Sweden Eva Nilsson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2022 walipofika Makao Makuu ya chama cha wasioona Tanzania.
Katibu Mkuu wa Chama wasioona Tanzania (TLB) Udageja Manonga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 12, 2022. wakati wakati wa kujadiliana namna za kuwawezesha watu wasioona pamoja na watoto wenye ualbino.
Mratibu Idara ya Wanawake na watoto wa Chama cha wasioona Tanzania (TLB), Subira Shedangio akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 12, 2022. wakati wakati wa kujadiliana na wanachama wa chama cha wasioona nchini Sweden namna za kuwawezesha watu wasioona pamoja na watoto wenye ualbino.

Wanachama wa chama cha wasioona Tanzania na Sweden na wasaidizi wao wakijaliana jambo.
Wanachama wa chama cha wasioona Tanzania na Swedeni na wasaidizi wao wakifurahia jambo.


CHAMA cha wasioona Tanzania wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwashirikisha kutoa maoni katika Sensa inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 nchini kote.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Chama wasioona Tanzania (TLB) Udageja Manonga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Agosti 12, 2022. Amesema kuwa hiyo ni matokeo ya serikali kuwaamini watu wasiiona nchini kupitia chama cha wasioona.

Pia Udageja ameishukuru serikali kwa kuwashika mkono pale ambapo chama kilikuwa kikipitia changamoto mbalimbali kutokana UVIKO 19.

Amesema Serikali iliendelea kushikamana na TLB na kuendelea kukipa fursa chama hicho ya kufanya ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wasioona nchini.

"Tumefanya kazi zetu za ushaswishi na utetezi kwa namna zuri pasipo kuzuiliwa wala pasipo kubugudhiwa katika ngazi zote za serikali." Amesema Udageja

Amesema wanashirikishwa mambo mbalimbali ikiwamo kutoa maoni katika sensa ambayo iko mbioni kufanyika mwaka huu.

Hata hivyo Udageja ametoa wito kwa wadau wengine ambao hawajaambatana nao katika kuendeleza gurudumu la kuambatana na Chama cha wasioona ikiwa chama hicho kinapenda kufanya kazi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa wanazingatia taratibu za chama na taratibu za nchi.

Udageja amewashukuru chama cha Wasiiona cha nchini Sweden ambao wanashirikiana nao na hawakushitushwa na changamoto cha chama ambazo zilijitokeza.

"Wameendelea kutuamini na kutuunga mkono na kuendelea kututia moyo ili tuweze kusimama na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwa kuhamasisha watu wasiiona kuendelea kujiunga na chama ili chama kiendelee kufanya kazi shughuli zake. Amesema Udageja

Kwa Upande wake, Mratibu Idara ya Wanawake na watoto wa Chama cha wasioona Tanzania (TLB), Subira Shedangio amesema idara ya wananawake na watoto inawaunganisha wananwake na watoto nchini ili kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuweza juinua hadhi zao kimaendeleo na Uchumi.

Amesema Wanawake wameweza kuwahamasisha kujiunga na harakati za kisiasa na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Amesema idara yake inawashawishi wazazi wasiwafiche watoto wasioona ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwamwo elimu, Afya na Ulinzi.

Amesema akizungumzia mradi wa kudahili watoto wenye ualbino na wasioona wa haki yangu (MY RIGHT SRF) amesema kuwa wameweza kuwafichua watoto wasiiona na watoto wenye Ualbino na kumewaibua watoto wengi ambao walikuwa wanakosa haki ya kwenda shule na sasa wameanza kwenda shule.

Amesema Mradi huo wa MY RIGHT SRF ulianza mwaka 2019 kwa ufadhili wa Serikali ya Sweden ambapo upo katika Wilaya sita za Tanzania bara na Zanzibar.

Subira amewashukuru Chama cha wasiiona Sweden kwa Kufadhili mradi huo kwa sababu wazazi na watoto wengi wameweza kuamka na kuelimika na kuwasaidia watoto kupata haki zao za msingi.

Ametoa wito kwa wazazi, wanajamii na serikali za mitaa na vijiji wanapowaona watoto wasioona au walemavu wamefichwa waweze kuwatoa ili waweze kupata haki yao ya kielimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad