Benki ya NMB imeibuka kidedea
katika taasisi za kibenki na kifedha kwenye maonesho ya Nanenane
yaliyofanyika kitaifa mwaka huu mkoani Mbeya.
Mbali na kunyakua
tuzo hiyo ya kitaifa, benki hiyo pia iliibuka mshindi katika maonesho ya
kanda yaliyofanyika kanda ya Nyanda za Juu, Ziwa na Magharibi,
Kaskazini, Mashariki na Kati.
Akizungumza muda mfupi baada ya
kupokea cheti cha ushindi, Mkuu wa idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya
NMB, Isaac Masusu alisema tuzo hizo zinasisitiza dhamira ya benki hiyo
kwa kutoa huduma za kibenki na bidhaa zinazoendana na matakwa ya wateja.
Lakini
pia, aliongezea kuwa wataendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali
kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo na kuwa tayari wameshusha
kiwango cha riba mpaka tarakimu moja kwa wateja wake katika sekta ya
kilimo.
Maonesho ya Nane Nane yaliyowakutanisha wadau mbalimbali
wa sekta ya kilimo yalizinduliwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango
Agosti 1, 2022 na kufungwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment