TANZIA: Balozi Shani O. Lweno Amefariki Dunia - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 21, 2022

TANZIA: Balozi Shani O. Lweno Amefariki Dunia

 

Taarifa ya familia imeeleza kuwa Marehenu Balozi Lweno amefariki leo alfajiri Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu na mazishi yatafanyika leo saa kumi Alaasiri.


Balozi Shani Lweno alisoma Shule ya Tabora Boys miaka ya 1960 na baadaye kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka  1971 na mwaka huo huo aliajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje   kama Afisa Ubalozi Conakry - Guinea. Baada ya hapo alifanya kazi katika Balozi za Tanzania Cairo -  Misri, Khartoum -  Sudan, Stockholm - Sweden,  New York - Marekani na Addis Ababa - Ethiopia kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje. Mnamo mwaka 1993 aliteuliwa kuwa Balozi wetu Lusaka, Zambia mpaka alipostaafu  mwaka 2003.

Baada ya kustaafu Alijiunga na timu ya Kitengo cha Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika  iliyokuwa inasimamia Suala la Uhuru wa Sahara Magharibi.  Baada ya mkataba wake kumalizika alirejea nyumbani.  Balozi Lweno ameacha mke na watoto. 

Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad