Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza
na jamii ya wawindaji ya Wahdazabe katika kijiji cha Munguli kata ya
Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida alipokwenda kutoa hatimiliki
za kimila kwa wananchi wa jamii hiyo Juni 11, 2022. Wa pili kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.
Mkuu
wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida Sophia Kizigo akizungumza wakati
wa zoezi la utoaji hatimiliki za kimila kwa jamii ya wawindaji ya
Wahdazabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza Juni 11, 2022.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Mkuu wa
wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo wakiwapungia mkono wananchi wa jamii ya
wawindaji ya Wahdazabe wakati wa zoezi la utoaji hatimiliki za kimila
kwenye kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoa wa
Singida Juni 11, 2022.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpatia
hatimiliki ya kimila Chifu wa jamii ya wawindaji ya wahadzabe Edward
Mkumbo kwenye kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama
mkoani Singida Juni 11, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Mkalama Sophia Kizigo,
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Mkuu wa
wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo wakiwa katika picha ya pamoja na
wananchi wa jamii ya wawindaji ya Wahdazabe kwenye kijiji cha Munguli
kata ya Mwengeza mara baada ya kuwakabidhi Hatimiliki za kimila Juni
11, 2022.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka
kwenye nyumba ya Chifu wa Jamii ya wawindaji ya Wahadzabe katika kijiji
cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida Juni 11,
2022. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika
picha na Jamii ya wawindaji ya Wahadzabe katika kijiji cha Munguli kata
ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida mara baada ya kutembelea
nyumba ya chifu wa jamii hiyo wakati wa ziara ya utoaji hatimiliki za
kimila Juni 11, 2022.
Chifu
wa jamii ya wawindaji ya wahadzabe Edward Mkumbo akiwa amesishikilia
hatimiliki ya ardhi mara baadhi ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula katika kijiji cha Munguli
kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida Juni 11, 2022. (PICHA
NA WIZARA YA ARDHI)
************************
Na Munir Shemweta, WANMM MKALAMMA
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameipongeza
jamii ya wawindaji ya wahadzabe iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida
kwa utayari iliyouonesha wa kutambua na kukubali kupimiwa maeneo yao na
kupatiwa hatimiliki za kimila.
Jumla ya hatimiliki za kimila mia
moja (100) zikiwemo 26 zinazomilikiwa kwa pamoja kati ya mke na mume
zimetolewa kwa jamii ya wawindaji ya Wahadzabe ikiwa ni hatua kubwa
kutokana na jamii hiyo kujishughulisha zaidi na uwindaji, utafutaji
matunda, urinaji asali na uchimbaji mizizi.
Dkt Mabula alisema,
hatua hiyo inaonesha nia na dhamira njema waliyonayo ya kutaka kuyalinda
maeneo yao wenyewe na kwa kushirikiana na serikali.
‘’Hakika
hizi ni salamu na ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuwa jamii ya wawindaji inaungana naye na mkoa
tayari kwenda naye sambamba katika kuletea watu wote maendeleo’’ alisema
Dkt Mabula.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya wawindaji ya
Wahadzabe katika kijiji cha Munguli kata ya Mwengeza wilaya ya Mkalama
Juni 11, 2022 alisema, jamii hiyo ni miongoni mwa jamii ndogo nchini
ambayo iko katika hali ya kupoteza ardhi wanayoimiliki kutokana na jamii
nyingine kuingia na kufanya shughuli zisizoendana na tamaduni za jamii
hiyo jambo alilolieleza linahatarisha ustawi na maisha na desturi za
Wahadzabe.
‘’Katika miaka ya hivi karibuni jamii hii imekuwa
ikikabiliwa na tishio la kutoweka na kupoteza uhalisia wa maisha yao
baada ya jamii nyingine kuingia katika maeneo ya mapori ya asili
yanayotumiwa na Wahadzabe kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji,
ukulima na hata upasuaji wa mbao jambo alilolieleza limekuwa tishio kwa
kiasi kikubwa kwenye jamii hii’’ alisema Dkt Mabula
Alitolea
mfano wamatishio kwa jamii hiyo kuwa ni pamoja na kupotea kwa makazi ya
asili yanayojengwa kwa nyasi kavu chini ya matawi ya miti, wanyama
kutoweka, mizizi na matunda kupotea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
na shughuli nyingine ambazo hazilindi uoto wa asiili wa mapori hayo.
Hata
hivyo, alisema kuwa, kwa kutambua athari iliyopo mbele ya jamii hiyo ya
wahadzabe, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa
ikitafuta njia bora ya kulinda jamii hiyo pamoja na jamii nyingine
zinazofanana ili kuhakikisha inajenga jamii yenye usawa kwa watumiaji
wote wa rasilimali za ardhi nchini.
Aidha, katika kuleta usawa
Serikali imeendelea na program mbalimbali kuhakikisha kila kipande cha
ardhi kinapimwa kwa lengo la kuruhusu usawa na ustawi siyo tu wa
binadamu bali wa viumbe vyote vyote hai nchini.
‘’Ukiachilia
mbali ukuzaji na uhifadhi wa tamaduni za jamii ya uwindaji
kiloichonifurahisha zadi ni kuona jinsi jamii ilivyostaarabika kwa kuona
na kuelewa umuhimu wa baba na mama kumiliki ardhi kwa pamoja , kwa hili
niwapongeze’’ alisema Dkt Mabula.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama
Sophia Kizigo alisema, jamii ya Wahadzabe katika eneo hilo la kijiji cha
Munguli kata ya Mwengeza imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya mgogoro
wa mpaka unaosababisha maeneo wanayotegemea kwa shughuli zao kuharbiwa.
‘’Changamoto
kubwa ya hapa, jamii ya Wahadzabe vyakula wanatoa porini, wanakula
asali na nyama zakuwinda na misitu ikiharibiwa au maeneo wanayotegemea
kupata vyakula yanapoharibiwa ni changamoto kubwa, hata hivyo
niwapongeze kwa uvumilivu wao’’ alisema Kizigo.
Bosco Charles
Samweli, Diwani wa Kata ya Mwengeza alimueleza Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula kuwa, eneo hilo la jamii ya Wahadzabe
kwa muda mrefu limekuwa na changamoto ya migogoro ya mpaka na wananchi
wanaoishi wilaya za jirani za Karatu Arusha na Mbulu mkoa wa Manyara.
Hata hivyo alisema kwa sasa changamoto zinaelekea kumalizika kutokana na
juhudi kubwa za mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo katika kutafuta
ufumbuzi wa migogoro hiyo.
Monday, June 13, 2022

WAZIRI DKT MABULA AIPONGEZA JAMII YA WAHADZABE KWA KUKUBALI KUPIMIWA ARDHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment