Na Mwandishi Wetu Iringa
WADAU
wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika kongani ya Ihemi
inayoshughulikia mikoa ya Iringa na Njombe wameeleza mafanikio
waliyopata kwa Wafadhili wa Kituo cha kuendeleza kilimo nyanda za juu
kusini mwa Tanzania (SAGCOT) mara walipotembelea katika kongani hiyo
kujionea shughuli zinazofanyika katika kukuza na kuendeleza kilimo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mara baada ya kutembelewa na wafadhili hao ambao ni
Serikali ya Tanzania, ofisi ya Ubalozi wa Ufalme wa Norway, USDA/USAID,
FCDO (zamani UK AID), Wanufaika kutoka Kiwanda cha kuzalisha maziwa
cha Asas Dairies ltd, GBRI Business Solutions (T) Ltd, na Tamu Tamu
Tanzania wameeleza namna SAGCOT ilivyoweza kushirikiana nao katika
kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo kwenye ukanda huo na kuleta mchango
chanya katika pato la Taifa.
Afisa
ugani wa Kampuni ya Tamu Tamu Tanzania, Bw. Gibson Kalyetekela
alisema toka waanze kufanya kazi na SAGCOT mwaka 2019 kama wabia
wamepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwafikia wakulima zaidi ya elfu
kumi ambao wamenunua miche ya tufaa inayozalishwa na kampuni hiyo
sambamba na kuwapa na kutoa elimu kwa wakulima juu ya kilimo cha zao.
“Kupitia
Sagcot tumeweza kuwafikia wakulima 10,000 ambapo tumekuwa tukiwapa
elimu juu ya usimamizi wa kilimo cha zao hilo, sambamba na kuwaelimisha
juu ya kupima afya ya udongo ili kubaini mapungufu yaliyopo kwenye
udongo ili kuurutubisha na kutoa mavuno mazuri,” alisema Bw.Kalyetekela
Aliwaeleza
wageni hao kuwa kampuni yao imejipanga kuwafikia wakulima 30,000 kwa
mwaka huu kwa kuwapa elimu juu ya maandalizi ya ardhi kwa kilimo,
umuhimu wa kupima afya ya udongo na matumzi sahihi ya chokaa mazao na
kuwapatia miche bora ya tufaa ili waweze kupata mavuno mazuri na kupiga
hatua kiuchumi na maendeleo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS, Bw. Fuad Abri
alisema Kituo cha Sagcot kimekuwa ni kiunganishi kati ya wakulima,
wafugaji na masoko pamoja na watoa huduma za ugani kama pembejeo, mbegu
na zana za kilimo jambo lilopelekea mafanikio makubwa kwa wakulima na
wafugaji katika ukanda huu.
“SAGCOT
imetuwezesha kuwafikia wafugaji wengi katika mikoa ya Iringa, Njombe na
Mbeya jambo lililowezesha kiwanda kupata maziwa mengi kwa ajili ya
kusindika na kuwapa uhakika wa soko la maziwa ya wafugaji katika kongani
ya Ihemi,” alisema Bw.Abri
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GBRI Business Solutions ltd, Bi.Hadija
Jabir anayejihusisha na kilimo cha mboga na matunda mkoani Iringa
alishukuru kutembelewa na wabia hao na kusema Sagcot ni nguzo muhimu
katika mafanikio ya kampuni yake kwa kuiwezesha kufikia masoko ya ndani
na nje ya nchi.
‘’Kupitia
SAGCOT mpaka sasa nimeweza kufanya kazi na wakulima zaidi ya Elfu tano
wamboga na matunda na wauzaji kwenye magenge 840 katika mikoa ya Iringa
na Dar es salaam, jambo ambalo limeweza wakulima wengi kupiga hatua
kimaendeleo kupitia biashara hii,” alisema Bi.Jabir
Bi.
Jabir alisema SAGCOT imeweza kuwakutanisha na wadau mbalimbali
ikiwa ni pamoja na wadau wa maendeleo, mabenki pamoja na kuwajengea
uwezo kwenye upande wa biashara kwa kuwaunganisha na wadau ambao
wameshafanikiwa kwenye biashara.
Taasisi
ya SAGCOT inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania, Mashirika ya Misaada ya
kimataifa hususani Ubalozi wa Ufalme wa Norway, USDA/USAID na FCDO
(zamani UK Aid), Pia wamekuwa wakishirikiana na wadau wengine wa
maendeleo ya kilimo AGRA na kuunda ubia namashirika ya WWF na IUCN.
Daktari
wa Mifugo,Sikili wa ASAS DAIRIES FARM LTD (kushoto) akiwawaelezea
Wafadhili wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa
Tanzania (SAGCOT) namna ufugaji unavyofanywa kwenye shamba lilopo
Nyang'olo Wilayani Iringa waliokuwa kwenye ziara ya siku tatu kujionea
maendeleo kwenye Kongani ya Ihemi mwishoni mwa wiki (katikati) ni
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi SAGCOT, Bw. Ally Laay, kushoto kwake
ni Mkuu wa Kongani na Maendeleo ya Ubia, Bi. Maria Ijumba wapili kulia
ni Mkurugenzi wa Fedha Bi. Anna Mtaita.

Mkurugenzi
wa kiwanda cha maziwa cha ASAS, Bw. Fuad Abri katikati akizungumza na
wabia, Menejimenti ya SAGCOT mara baada kutembelea Shamba
linalomilikiwa na kampuni hiyo lililopo kitongoji cha igingilagwa
mwishoni mwa wiiki Mkoani Iringa Ikiwa ni ziara ya siku tatu ya
Wafadhili wa Kituo cha kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa
Tanzania (SAGCOT), wa kwanza kushoto ni Meneja Kongani ya Ihemi Bw.
Hkalid Mgalamo , Wapili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Bw.
Geoffrey Kirenga na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Bi. Anna
Mtaita.
No comments:
Post a Comment