HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 8, 2022

TAFITI ZINAONYESHA CHANJO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UVIKO 19

 

Na Mwandishi Wetu
SHANJO ni njia Bora zaidi ya kujiandaa na mawimbi mapya ya ugonjwa wa UVIKO 19 katika kipindi ambacho dunia inaendelea kupigana vita dhidi ya kirusi hatari cha Korona.

Takribani nchi zote zinaendelea kuwapatia chanjo wananchi wake ili kuweza kujikinga dhidi ya UVIKO 19 na kupunguza kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo.

Dkt. Kunda Steven ambaye ni Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Afya nchini (NIMR) alisema haya wakati alipofanya mahojiano na timu ya Amref Health Africa Tanzania ambapo alieleza kuwa umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo za Korona kwani tafiti tayari zinaonyesha kuwa chanjo ina mchango mkubwa sana katika kupunguza kasi ya maabukizi ya UVIKO 19.

Dkt. Kunda aliendelea kusema kuwa endapo ikatokea nchi ya Tanzania kupatwa na wimbi jingine la ugonjwa huu basi chanjo ndiyo njia bora zaidi ya kujiandaa na mawimbi mengine yanayoweza kutokea.

"Ukiachana na faida ambazo wanazipata leo watu waliochanja kama kutopatwa na ugonjwa mkali endapo wataambukizwa Korona, watu hawa pia watakuwa katika nafasi nzuri sana ya kupambana na mawimbi mapya pale yatakapotokea"alisema Dkt. Kunda.

"Dunia tayari imeshuhudia mawimbi takribani manne ya kirusi cha Korona na madhara yake tayari tumeyaona ambavyo yamekuwa makubwa"alisema Dkt. Kunda Aliendelea kwa kusema kuwa hivyo kama Taifa ni vema tukaendelea kujiandaa kwa kuhakikisha kuwa tunachanja chanjo za UVIKO 19 ambazo zinatolewa kwenye Hospitali kote nchini pamoja na Vituo maalumu.

"Ni vema pia kuendelea kuwasikiliza wataalamu wetu wa afya ambao kwa kupitia Taasisi kama Amref Health Africa Tanzania wamekuwa wakipewa nafasi ya kutoa elimu kwa jamii na kufikisha ujumbe ambao utaisaidia jamii ya watanzania kuendelea kuwa salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad