• Teknolojia hii ya EDX
hurahisisha uchakataji na uwasilishaji wa taarifa za wakopaji kwa
taasisi za kifedha kwa njia ya kielektroniki.
•
Uwasilishaji wa taarifa za wakopaji kwa njia hii ya kisasa
utarahisisha mtiririko wa kazi kwa taasisi husika, kupunguza makosa
pamoja na kusaidia taasisi kufuata kanuni na sheria za Benki Kuu ya
Tanzania za ukusanyaji wa taarifa za mikopo.
Taasisi ya Dun
& Bradstreet Bureau Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Dun &
Bradstreet Credit Bureau Limited, leo imetanganza kuzindua teknolojia
mpya yenye uwezo mkubwa wa kuchakata, kusafirisha na kuwasilisha taarifa
kwa haraka inayojulikana kama EDX.
EDX
ni maalum kwa taasisi za kifedha zinazotoa mikopo pamoja na
uwasilishaji wa taarifa za wakopaji kwenda kwenye kanzi data ya Benki
Kuu ya Tanzania. EDX itasaidia taasisi za kifedha kuondoa makosa wakati
wa uwasilishaji wa taarifa hizo, kuokoa gharama pamoja na kutoa taarifa
sahihi pale zinapohitajika.
EDX ni teknolojia ambayo hurahisisha
uchakataji na uwasilishaji wa taarifa za wakopaji kwa taasisi za kifedha
kwa njia ya kielektroniki. Vile vile, uwasilishaji wa taarifa za
wakopaji kwa njia hii ya kisasa utarahisisha mtiririko wa kazi kwa
taasisi husika, kupunguza makosa pamoja na kusaidia taasisi kufuata
kanuni na sheria za Benki Kuu ya Tanzania za ukusanyaji wa taarifa za
mikopo.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza uzinduzi wa EDX, Meneja wa
taasisi ya Dun & Bradstreet Tanzania Junaid Malik alisema
‘Teknolojia ni moja ya nguzo kuu kwa taasisi za kifedha na benki.
Hata hivyo, uwepo wa teknolojia hii katika sekta umesababisha kuongezeka kwa idadi ya taarifa zinazohifadhiwa, usimamizi wa taarifa pamoja na ongezeko la mahitaji ya taarifa kutoka kwa wasimamizi wa sekta ya fedha. EDX hurahisisha uchakataji wa taarifa kieletroniki ili taasisi za kifedha ziweze kuzituma katika mfumo unao stahili wakati wa upelekaji wa taarifa za wakopaji kwa kwa Benki Kuu ya Tanzania pale zinapohitajika”.
Malik
aliongeza “Tumeweza kuweka mtiririko wa taarifa kuwa wa kieletroniki
ili uwasilishaji wa taarifa kuwa wa kisasa, hakuna sababu ya kujiongezea
gharama za teknolojia mfumo huu unakupa uhakika kwa kuzingatia vigezo
na kanuni za ukusanyaji na uwasilishaji wa taarifa za mikopo kwa
usahihi. Unaweza kutoa taarifa kutoka kwenye vyanzo tofauti ukaziweka
pamoja kwa kufuata taratibu za biashara yako kisha ukaziweka kwenye
muundo wowote unaotakiwa kulingana na kanuni na sheria za Benki Kuu ya
Tanzania.
Wataalamu wa Dun & Bradsheet Credit Bureau Tanzania
watasaidia kwenye uunganishaji wa EDX. Baada ya EDX kuunganishwa kwenye
taasisi husika, mfumo huo utaendelea kufanya kazi kielektroniki.
EDX
itahakikisha uwasilishaji wa taarifa kwa usahihi, kwenye muonekano
mzuri kwa watumiaji na kutoa ripoti ya kina. Vipengele hivi hutoa uwezo
kwa watumiaji kutathmini mtiririko mzima wa uwasilishaji wa taarifa
pamoja na kurekebisha, kuthibitisha vyanzo vya taarifa hizo kwa
kuzingatia uhitaji.
Malik alisema kuwa EDX inasaidia kuokoa
gharama za uendeshaji kwa zaidi ya asilimia 75%, ni rahisi na haraka
kuunganisha inachukua muda mfupi usiozidi wiki tatu huku miundombinu
yake ikichukua nafasi ndogo zaidi kama teknolojia ya Kubernetes.
‘EDX
pia inasaidia kufikia vyanzo vingi vya taarifa, kuwasilisha, kuhakiki
na kuchapisha kwenye muundo wowote. Inapunguza uingizaji wa data kwa
mkono kwa asilimia 90%, kutoa taarifa kwa wakati na kupunguza kupoteza
muda kwa zaidi ya asilimia 85%’ alisema Malik.
EDX inapatikana
kwa manunuzi kutoka Dun & Bradsheet Credit Bureau Tanzania. Kwa
maelezo Zaidi wasiliana nasi kupitia namba +255 222 135 445.
No comments:
Post a Comment