HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 7, 2022

Benki ya I&M yatoa msaada kwa shule ya msingi ya Mtongani

 
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mtongani iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, sasa wataweza kusoma kwenye mazingira bora baada ya beki ya I&M kutoa msaada wa madawati 100 ambayo yataweza kunufaisha wanafunzi 300 pamoja na vifaa vya usikivu 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia. Vilr vile, wanafanyakazi wa benki hiyo wameungana kutoa msaada kwa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye uhitaji wa shule hiyo. 


Msaada huo wenye thamani ya Tzs12.5 milioni umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo kwa niaba ya Shule y Msingi ya Mtongani. Msaada huu kutoka kwa benki ya I&M ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata masomo yao kwenye mazingira rafiki.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara benki I&M Lilian Mtali alisema kuwa msaada huo una lengo la kutengeneza fursa kati ya wafanya biashara na jamii inayozunguka.

‘Fursa sio kwa ajili ya fedha tu, ni kutengeneza maisha ya baadae kwa watu pamoja na jamii sehemu yeyoye duniani’, alisema Mtali.

Mtali aliongeza ‘Maono ya benki ya I&M ni kutoa hamasa na kusaidia kubadilisha maisha ya Watanzania kila siku. Tunafanya biashara kwa njia sahihi na kwa ajili ya maisha ya baadae, msaada huu kwa shule ya Msingi ya Mtongano utawapa nafasi ya mafanikio kwenye elimu yao.

Alisema ushirikiano baina ya sekta binafsi, serikali pamoja na taasisi zisizo za serikali ni njia bora kabisa ya kutatua changamoto zinazowakabili maisha ya Watanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo alisema kuwa msaada huu uliotolewa na benki ya I&M unaonyesha ushirikiano mzuri uliopo baina ya serikali na sekta binafsi, ambao kwa kiasi kikubwa umeweza kunufaisha jamii kwani madawati haya yataweza kutatua changamoto ya wanafunzi kukaa chini ambayo ilikuwa inawakabili kwa muda mrefu.

‘Msaada huu tuliopokea leo kutoka kwa benki ya I&M kwa ajili ya shule ya Msingi ya Mtongani unaonyesha ni kwa jinsi ngani serikali inavyofanya kazi kwa ukaribu na sekta binafsi kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania siku hadi siku.

Akizungumza mara ya kupokea msaada huo, Mwali Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mtongani Victor Kangahti alishukuru benki ya I&M huku akisema msaada huo umekuja muda muafaka kwani shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba ya mawadati kufuatia ongezeko la wanafunzi mara baada ya serikali kutangaza elimu ya bure.

Kwa niaba ya uongozi wa shule yetu, naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza benki ya I&M kwa msaada huu kwa shule yetu. Mimi kama Mkuu wa Shule hii, naomba niwaakikishie ya kwamba msaada huu wa madawati utatumika vyema kama ilivyokusudiwa pamoja na kutunza vizuri kwa ajili ya wanafunzi waliopo kwa sasa na kwa wale ambao watakuja kwa baadae.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Reja Reja wa benki ya I&M Lilian Mtali akimkabidhi baadhi ya vifaa vya usikivu kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo kwa niaba ya uongozi wa shule ya msingi ya Mtoni. Benki ya I&M ilitoa msaada wa madawati 100 pamoja na vifaa vya usikivu 50 kwa shule ya Msingi ya Mtoni ikiwa ni juhudi za kuunga serikali kuhahakisha kuwa wanafunzi wanapata elimu kwenye mazingira bora na rafiki.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Reja Reja wa benki ya I&M Lilian Mtali akijaribu kumvalisha kifaa cha kusikia mwanafunzi wa darasa la nne Abdul Juma wa shule ya Msingi ya Mtoni baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 100 pamoja na vifaa vya usikivu 50 kwa shule ya Msingi ya Mtoni ikiwa ni juhudi za kuunga serikali kuhahakisha kuwa wanafunzi wanapata elimu kwenye mazingira bora na rafiki.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad