HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 26, 2022

MATUKIO KATIKA PICHA: CRDB BANK PAMOJA BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DODOMA

 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akiongoza matembezi ikiwa ni sehemu ya Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbali ikiwemo ile ya Soka, Pete na Kikapu,  jijini Dodoma Juni 25, 2022. Picha zote na Othman Michuzi.
Dodoma 25 Juni 2022 – Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Akson ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuandaa bonanza la pamoja la michezo lililopewa jina la “CRDB Bank Pamoja Bonanza” kwa mafanikiao makubwa pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kushiriki katika michezo na kujenga afya na kuhamasisha mshikamano kwa Watanzania katika shughuli za maendeleo.

Akizungumza katika bonanza hilo, Spika alisema kuwa bonanza hilo limeleta msisimko na mwamko mkubwa kulinganisha na miaka ya nyuma, ambapo mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka na kufanya maana na lengo halisi la mashindano hayo kupata umaarufu jijini Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
“Kwa mwaka huu tumeona hata ndugu zetu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na pia vijana wetu wa Bongo Flava ambao kwa pamoja wameleta msisimko mkubwa na kuleta ushindani, hongereni sana ndungu zetu Bemki ya CRDB kwa kuwa na maono makubwa hivi”. Alisema Tulia.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB inaipa kipaumbele michezo, kwani michezo ni afya, inaleta umoja na upendo, inawaleta pamoja Wafanyakazi wa Benki na wadau mbalimbali wa Michezo nchini. Hivyo Benki inatumia bonanza hilo kama sehemu tu ya kuisogeza karibu na Serikali, Bunge na wadau mbalimbali nchini ili kupata nafasi ya kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki inaweza kushiriki katika mipango ya maendeleo ya nchi na kuthibitisha kauli mbiu yake ya “Ulipo Tupo” na kuwa ni benki inayomsikiliza Mteja. 
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Ally Laay aliwashukuru Wabunge na wadau mbalimbali wa serikali na wananchi waliohudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo lililotanguliwa na  matembezi yaliyo anzia katika viwanja vya bunge vikiwemo vikundi mbalimbali vya Jogging, wanafunzi wa vyuo na Sekondari pamoja na wananchi kwa kutambua umuhimu wa michezo.

Mashindano hayo yalimalizika kwa Timu za Bunge la Jamhuri wa Muungano kutwaa ushindi wa jumla kwa Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Pete pamoja na Ule wa kuvuta kama (Tag of War) katika bonanza hilo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kushoto) akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na viongozi wengine wakiongoza mazoezi ya viungo muda mfupi baada ya kumaliza matembezi 'CRDB Bank Pamoja Bonanza', yaliyoanzia kwenye viwanja vya Bunge na kuishia kwenye Uwanja wa Jamhuri na kufuatiwa na Michezo Mbalimbli ikiwemo ile  ya Soka, Mpira wa Pete, Kikapu nk.  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akizungumza katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza wakati akitoa salamu za mkoa katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022. 
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akionyesha uwezo wake katika kutimua mbio za mita 100 ambapo aliwaacha kwa umbali usiopikima kikawaida, Waheshimiwa Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akifurahi pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita, wakati akipokea medali yake baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za mita 100, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Cosato Chumi baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Picha ya pamoja na Mabingwa wa CRDB Bank Pamoja Bonanza.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Mhe.  katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Ridhiwani Kikwete katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi medali, Nahodha wa Timu ya Bunge ya mpira wa pete, Mhe. Mama Salma Kikwete, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimvisha medali, Mhe. Mama Salma Kikwete, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022. 






Mashindano ya kuvuta kamba kati ya Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mchezaji mahiri wa mpira wa pete wa timu ya Bunge, Mhe. Mama Salma Kikwete akiwaonyesha kazi timu ya Baraza la Wawakilishi, katika Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akitafuta nafasi wakati wakiwapelekea mashambulizi wapinzani wao, wakati wa Bonanza la Pamoja la Benki ya CRDB (CRDB Bank Pamoja Bonanza), lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri,  jijini Dodoma Juni 25, 2022.





 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad