HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 26, 2022

ALIYEKUMIWA MWAKA MMOJA KWA KUMTUSI MAMA YAKE MZAZI AACHIWA HURU

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Rar Es Salaam, imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala dhidi mfanyabiashara Zariina Mohamed Sidiki ambaye alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Gerezani kwa kumtukana mama yake mzazi.

Uamuzi hio umetolewa hivi karibuni na Jaji Juliana Masabo wa mahakama hiyo baada ya mshtakiwa kushinda rufaa yake aliyoikata mara tu baada ya kuhukimiwa Agosti 26, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mpaze

Akisoma uamuzi huo, Jaji Masabo amesema ameangalia na kuzingatia kuwa hukumu iliyotolewa ilikuwa na mapungufu ya uchambuzi wa ushahidi na kwamba mshtakiwa hakuwa na kosa hivyo anamuachia huru.

Akichambua hukumu hiyo, amesema Mhakama ya Ilala ilikosea kumtia hatiani na kumfunga mshtakiwa kwa kuwa mashtaka dhidi yake hayakuthibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote

Amesema, Mahakama hiyo pia ilikosea kumtia hatiani na kumfunga kwa sababu kulikua hakuna ushahidi uliotolewa dhidi ya mshtakiwa na kwamba mahakama haikuchambua ipasavyo ushahidi kwani ushahidi wa upande wa mashtaka haukuwa na uhakika.

Akiendelea kuchambua Hukumu hiyo Jaji Masabo amesema, ushahidi wa mshtakiwa haukuzingatiwa na ushahidi wa mashtaka ulikuwa wa kusikia tu na siyo wa kuungana.

Amesema, mashtaka dhidi yake mshtakiwa hayajulikani kwamba alitoa lugha ya matusi dhidi ya mama yake Novemba 29,2019 lakkni hayakufafanua muda gani alitoa lugha hiyo ya matusi.

Amesema katika utetezi wake, mrufani alidai kuwa wakati akitoa lugha hiyo ya matusi mteja wake alikuwepo lakini mteja wake huyo hakuitwa kuja kutoa ushahidi mahakamani na kwamba kitendo cha kutokuitwa kwa shahidi huyo ambaye alikuwa ni shahidi wa muhimu katika kesi hiyo, kunafanya mashtaka dhidi mshtakiwa kutothibitika.

Jaji alienda mbali zaidi na kusema, zaidi kuwa dukani hapo kilikuwa na na CCTV kamera, ilitegemewa ya kwamba Upande wa mashtaka wangeuwasilisha ushahidi huo lakini haukufanyika hivyo.

Jaji Masabo amesema, kumbukumbu za kesi inaonyesha mzizi wa mashtaka hayo ni matatizo ya kifamilia na biashara kwani inaonyesha kuwa, mrufani, mlalamikiwa na mashahidi wote ni ndugu .

Aidha katika utetezi wake, Mrufani anadai kesi hiyo ni ya kupandikizwa kwa kuwa inahusiana na mambo ya kifamilia na biashara na kwamba ndugu zake wanataka kumtia kwenye group biashara zake.

Mahakama baada ya kusikiliza pande zote mbili, yaani mrufani na mjibu rufani mahakama imesema... Ninakukubaliana na wakili wa mrufani kwamba kes si dhidi ya mrufani haijathibitishwa hivyo rufaa inakubaliwa hivyo hatia na kifungo dhidi ya mshtakiwa imeondolewa na imemriwa ya kwamba aachiwe labda kama anashtakiwa na kesi nyingine kisheria.

Akizungumza nje ya Mahakama baada ya kuachiwa huru Zarina ameshukuru kuwa haki imetendeka kwa kuonekana kuwa hana hatia.

"Nawashauri wanawake wenzangu walioachiwa familia wasikate tamaa, wale wenye tabia ya kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake waache kufanya hivyo, waache wanawake wanaotunza familia watimize majukumu yao.

Nimekutana na changamoto nyingi za kudidimiza hata ndani ya familia kwa sababu na mimi ni mwanamke niliyetekelezwa natunza familia yangu yenye watoto watano na wajukuu wawili lakini nashukuru nimekuwa jasiri na naamini nitashinda." Amesema Zarina

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad