HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 26, 2022

WANAWAKE KKKT USHARIKA WA BOKO WATOA MSAADA KWA WATOTO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

 Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Boko, Marry Kombe (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zuhura Mawona, sehemu ya zawadi zilizotolewa na Wanawake wa KKKT Usharika wa Boko. Vitu vilivyokabidhiwa ni jokofu moja, mashuka 100, viyoyozi (AC) viwili, pamoja na kifaa cha kuzuia moto katika jokofu vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4.4.


UMOJA wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko Jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2022 wamewatembelea na kuwafariji watoto wanasumbuliwa na maradhi ya saratani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha watoto wanaougua saratani.

Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zuhura Mawona (kushoto), akizungumza wakati wa kupokea zawadi zilizotolewa na Wanawake wa KKKT Usharika wa Boko kwa ajili ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika hospitali hiyo. Vitu vilivyokabidhiwa ni jokofu moja, mashuka 100, viyoyozi (AC) viwili, pamoja na kifaa cha kuzuia moto katika jokofu.
Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Mchungaji Kiongozi Ambakisye Lusekelo, Mwinjilisti wa kanisa hilo, Marry Kombe, amesema kuwa mbali ya kuwafariji watoto hao, pia wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo jokofu moja, mashuka 100 pamoja na viyoyozi (AC) viwili, pamoja na kifaa cha kuzuia moto katika jokofu vikiwa na thamani ya shilingi milioni 4.4 ambavyo vimekabidhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo.
 Aidha Mwinjilisti Marry amesema kuwa Wanawake wa KKKT Usharika wa Boko wamekuwa na utamaduni wa kujitoa kwa kuchangishana na kupeleka mahitaji mbalimbali kwa watoto wanaopata matibabu ya saratani.

“Kipekee tuwashukuru wanawake wa Boko kwa wazo ambalo walikuwa nalo, wakachangishana wakatoa kwa moyo mkunjufu na kwa moyo wa kupenda na kuungana kwa pamoja na kuleta hii sadaka hapa muhimbili.” alisema na kuongeza kuwa urafiki kati ya watoto hao na umoja huo ulianza kwa kutoa huduma ya kujitoa matendo ya huruma kuanzia mwaka 2018 na imekuwa endelevu.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili, Mkurugenzi Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Zuhura Mawona, amewashukuru Wanawake wa KKKT, Usharika wa Boko kwa zawadi walizotoa ambazo ni jokofu, mashuka 100, viyoyozi (AC) mbili pamoja na kifaa cha kuzuia jokofu lisiungue ambavyo vitaweza kusaidia kutoa huduma nzuri kwa watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani hospitalini hapo.

Zuhura ametoa rai kwa wadau wengine kuwatembela na kutoa msaada wa hali na mali ambayo itasaidia kutoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili. katika kuiga mfano wa wanawake hao katika kujitoa kwa moyo kwani wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka.

“Hospitali kama hospitali tumebeba majukumu makubwa kuhakikisha kwamba kila rasilimali iliyopo inatumika kusaidia wagonjwa pamoja na wateja wote wanaokuja hospitali, hizi zawadi na misaada ya hali na mali tunayoipata tunaona njia mojawapo ambayo kwanza inatuweka karibu na jamii ambayo inatusaidia sisi kama wataalamu kutoa huduma kwa wateja wetu. Alisema.

Mkurugenzi huyo amewashukuru Wanawake wa KKKT usharika wa Boko na kusema kuwa msaada wao utaenda kuwapa faraja watoto wanaoendela na matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad