HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWASILI NCHINI SWEDEN

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 31 Mei 2022 amewasili Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajia kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Juni 2022 nchini humo.

Dhumuni la mkutano huo ni kuchochea utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (Ajenda 2030) hususani katika upande wa mazingira na kujadili namna ya kurejesha uchumi endelevu katika kukabiliana na janga la Uviko 19. Aidha mkutano huo ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika mkutano wa kwanza wa mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Stockholm mwaka 1972.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wadau wa Mazingira Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad