Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akieleza
jambo wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu
mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea
kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za
Bunge, jijini Dodoma.

Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (Mb) akielezea masuala ya
ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa wa
Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao
kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma, kushoto ni Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na kulia ni
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa.

Waziri
wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) akieleza jambo wakati wa
kikao na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji
wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya
Serikali, kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.

Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Abbas Tarimba, akizungumzia maendeleo ya jimbo lake, wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.

Mbunge
wa Kigamboni na Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam, Dkt.
Faustine Ndungulile, akifafanua jambo wakati wa kikao na Wabunge wa Mkoa
wa Dar es Salaam, kuhusu mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
katika mkoa huo kuelekea kwenye Bajeti Kuu ya Serikali, kikao
kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, jijini Dodoma.

Kikao
cha Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi na Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Ofisi za Bunge,
jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
No comments:
Post a Comment