Na Mashala Mhando, Muheza
MBUNGE
wa jimbo la Muheza, Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA, jana alinogesha
usiku wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali
zilizompa umaarufu kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Mbunge
huyo ambaye alikonga nyoyo za vijana na watu wengine waliokuwa kwenye
mkesha huo uliohidhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya baada ya
kumaliza mbio zake katika wilaya hiyo.
Nyimbo
alizoimba na kuwaacha hoi, mamia ya watu waliojazana kwenye uwanja wa
Jitegemee mjini hapa ni pamoja na wimbo 'Kwa Mungu hakuna majungu, wee
Endelee tu' na 'Asante kwa Kuja'.
Nyingine
ambazo hapan'shaka zilivuya hisia za watu waliojazana kwenye uwanja huo
ni pamoja na wimbo 'Binadamu Kukunja Goti' alioamshirikisha AY,
'Mfalme' alioimba na G Nako pamoja na wimbo mpya wa 'Gwiji Remix'.
Watu waliohudhuria mkesha huo, walisema amekomaa katika nyanja ya siasa pamoja na majukumu yake ya kuimba muziki.
"Kiukweli
acha niwe mnafki, mbunge wetu anaupiga mwingi, bungeni anawasha moto
kwa hoja zake za kisiasa kututetea wana-Muheza na leo hii ametupa
burudani ya kutosha kabisa, hongera zake," alisema Ramadhani Sebwijo
mkazi wa Kicheba Muheza.
Naye
John Mdami mkazi wa Kerenge Muheza alisema kitendo cha mbunge wao kutoa
burudani kunogesha mkesha wa Mwenge, kimesaidia kuongeza alama katika
shamra shamra za mwenge huo.
"Hakika
tumepata Mbunge, hapa ametupa burudani ya kufa mtu, juzi nimemsikia
bungeni akichangia mjadala wa Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya
Makazi, alitutetea sana kuhusu mashamba ya chai yaliyotelekezwa akaiomba
serikali itupe tupate maeneo ya kulima," alisema Mdami na kuongeza,
"Tumechagua mbunge anayekidhi mahitaji yetu ya burudani, kisiasa na kijamii,".
Mkuu
wa wilaya Halima Bulembo aliwakumbusha wananchi waliofika kwenye mkesha
huo, kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu
na makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu.
"Pamoja
na burudani mnayoipata kutoka kwa mbunge wenu msisahau ujumbe uliotolea
na Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu Sahil Geraruma, mjitokeze
kwenye sensa," alisema mkuu huyo wa wilaya.
Mwenge
ulipitia na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ipatayo minane
kwenye wilaya hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7
No comments:
Post a Comment