HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 24, 2022

MATAPELI WA ARDHI MKOA WA PWANI WAPEWA ONYO

 

Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Christopher Myava akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani leo Mei 24,2022.

Na Khadija Kalili, Pwani
Kamanda Mkoa wa Pwani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Christopher Myava ametoa onyo kali kwa matapeli wanaouchafua Mkoa wa Pwani kutokana na migogoro ya uuzwaji wa zaidi ya mara moja wa Ardhi Mkoani hapa.

Kamanda Myava ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

"Tumedhamiria kupambana na matapeli hawa kwa sababu migogoro ya uuzwaji wa Ardhi isivyo halali ndani ya Mkoa Pwani imekithiri na hasa Wilaya ya Bagamoyo sisi TAKUKURU tunasema tuko kazini na tutawapatia dawa" alisema Kamanda Myava.

Kamanda Myava alisema kuwa kutokana na kuwa na tatizo sugu la uzwahi kitapeli wa ardhi Mkoani Pwani huku matapeli hao wakishirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali, tatizo hili limekua sugu hivyo sisi hatuko tayari kuona Mkoa ambao unawavutia wawekezaji kuja kuwekeza ukichafuliwa na baadhi ya watu tunatembea na dawa tukikukamata tunampatua muhusika bila mawaa" alisema Kamanda huyo wa TAKUKURU Myava.

Amesema kuwa anatoa onto kwa wote wenye nia mbaya ya kuihujumu Serikali kwenye miradi ya maendeleo.

"Nadhani mmeshuhudia maafisa wa TAKUKURU wakipita kukagua miradi hiyo Kila wakati, tutakuwa wakali sana kwa watu wanaojihusisha na rushwa au ufisadi kwenye miradi hiyo ya maendeleo tuungane pamoja katika kuijenga Tanzania yenye maendeleo ya kweli kupitia miradi hii inayoanzishwa na serikali yetu" alisema Kamanda Myava.

Aidha akizungumzia kuhusu harakati za uchaguzi wa ndani wa baadhi ya vyama niwaombe sana tutumie fursa tuliyonayo kuchagua viongozi waadilifu na wenye nia ya kweli ya kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii.

Kamanda Myava alisema hayo alipokua akitoa ripoti ya kazi zilizotekelezwa na TAKUKURU Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu ambapo huu ni utaratibu wa Taasisi hiyo kufanya hivyo ili umma Watanzania uweze kumfahamu wanafanya nini ikiwa ni pamoja na kutambua vipaumbele vyao katika mapambano dhidi ya rushwa .

"TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamefanya mgawanyo wa maeneo makuu maneo ambayo ni katika sekta ya elimu na ujenzi ambapo walifanya uchambuzi wa mfumo kuhusu uchangishwaji wa michango kwa Shule za msingi kwa kupitia uchambuzi huu TAKUKURU kwa kushirikiana na wadau wa elimu wa Shule hizo walifanya kikao kazi(warsha) na kuweka maazimio ya kutekeleza Ili kuondoka changamoto au mapungufu yanayoweza kubainika katika zoezi la ukusanyaji wa michango hiyo.

Katika sekta ya ujenzi amesema walifanya uchambuzi wa mfumo wa utendaji kazi TEMESA na kubaini baadhi ya mapungufu madogo ambayo tayari TAKUKURU wameshakaa na wahusika na kuelekezana namna Bora ya kutatua au kuondoka mapungufu hayo.

"Katika robo ya mwaka, tumefuatilia jumla ya miradi ya maendeleo 182 katika sekta ya Afya, Elimu,Ujenzi na Maji miradi hiyo inathamani ya Bil.8 (8,478,941,500).

Amesema kuwa kwa robo hii ya mwaka Ofisi ilipokea jumla ya malalamiko 98 kati ya malalamiko hayo 51 yalihusu rushwa na malalamiko 47 hayakuhusu rushwa , malalamiko 51 ambayo yalihusu rushwa yalianzishiwa majalada ya uchunguzi ambao bado unaendelea, malalamiko 47 ambayo hayakuhusiana na rushwa walalamikaji 46 walielimishwa na kushauriwa ili kutatua tatizo husika na mlalamikaji mmoja taarifa yake ilihamishiwa idara ingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad