HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 29, 2022

MAKAMU NA UZINDUZI WA UPANDAJI MITI MASKULINI ZANZIBAR

 

 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Massoud Othman, amewataka wazanzibari kufanya  juhudi za pamoja katika suala la kupanda mititi ya aina mbali mbali ikiwemo ya matunda, biashara na kivuli  ili kuirejesha Zanzibar kuwa ya kijani. 

Mhe. Othman ameyasema hayo huko Skuli ya Mwera Wilaya ya Magharib Wilaya ya Kati Unguja alipozungumza katika hafla ya uzinduzi wa Siku ya Upandaji miti Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya Skuli za Unguja na Pemba.

Amefahamisha kwamba kufanyika kwa juhuzi za kupanda miti, pamoja na kuacha kukata miti ovyo, kutachangia na kuondosha athari zilizpo zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo imechangia maeneo mengi kuharibika.

Mhe. Othman amesema kwamba pia juhudi za upandaji miti ni muhimu kuendelezwa kwa kuwa mbali na kusaidia  kuirejesha Zanzibar kuwa ya kijani, lakini pia ni uchumi mkubwa kwa wananchi na pia kunapatikana mafuta, vyakula na ni rasilimali muhimu katika utengenezaji wa madawa mbali mbali ya binaadamu.

Amesema kutokana na hali hiyo, ni dhahiri kwamba Wazanzibari kama walivyo wengine wengi duniani hawawezi kuishi bila ya kuwepo miti na kuonya kwamba wasiendeleze tabia ya kuyageuza mapori kuwa majangwa kwa kukata miti ovyo jambo ambalo linaathari kubwa kwa nchi  na jamii kwa jumla.

Kutokana na hali hiyo, amesema kwamba serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar inampango mkubwa wa kuifanya Zanzibar kuwa ya kijani kwa kuanzisha mradi na program za upandaji miti ya aina mbali mbali ikiwemo ya matunda vivuli naya biashara katika skuli na maeneo  mengine yatakayohitajika kufanywa hivyo.

Ameitaka jamii kuendeleza mashirikiano na vyombo mbali mbali vya serikali na binafsi katika kuhakikisha kwamba suala la upandaji miti linapata msukumo  stahiki ili dhamira ya kuhakikisha Zanzibar inakuwa ya kijani iweze kufanikiwa.

Aidha amewakumbusha viongozi wa mikoa na wilaya kuhakikisha kwamba wanasimamia vyema suala la Mipango miji ili kuondosha ujenzi holela unaofanywa katika maeneo mbali mbali nchini.

Kwa upande mwengine Mhe. Othman alikumbusha haja ya kutunza historia ya nchi na kuuagiza uongozi wa Skuli ya Mwera kuhakikisha kwamba wanalitunza Darasa la Historia kwenye Skuli hiyo ambalo alisoma muasisi wa Mapinduzi Marehemu Abeid Amain Karume.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid,  amesema kwamba juhudi kubwa zinafanyika katika kushirikiana na taasisi na mamlaka mbali mbali ili hakikisha kwamba serikali inafanikiwa katika suala la upandaji wa miti.

Aidha amesema kwamba pia serikali inaendelea na juhudi kubwa za ujenzi wa  madarasa mapya ya skuli katika maeneo mbali mbali ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia sekta tofauti ikiwemo elimu.

Mapema Mhe. Othman katika uzinduzi huo alipanda mti wa Muembe katika Skuli ya Mwera na baadaye kutembelea mazingira ya skuli hiyo ikiwemo hali ya madarasa na kujionea changamoto mbali mbali za skuli hiyo.

Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Kitengo cha Habari leo tarehe 29/05/2022.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Othman Masoud Othman, akiwa ameshikilia mche wa Mti wa Mumbe akijitayarisha kuupanda katika hafla ya uzindizi wa upandaji miti Zanzibar . Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 29/05/2022 huko skuli ya Mwera wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa Chuo cha  Zanzibar Microtech Farhia Mohammed Ali. ( Picha na Ofisiya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Othman Masoud Othman, akiweka mchanga baada ya kupanda mche wa Mti wa Mumbe katika hafla ya uzindizi wa upandaji miti Zanzibar . Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 29/05/2022 huko skuli ya Mwera wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa Chuo cha  Zanzibar Microtech Bi Farhia Mohammed Ali. ( Picha na Ofisiya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Othman Masoud Othman, akiweka mchanga baada ya kupanda mche wa Mti wa Mumbe katika hafla ya uzindizi wa upandaji miti Zanzibar . Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 29/05/2022 huko skuli ya Mwera wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa Chuo cha  Zanzibar Microtech Bi Farhia Mohammed Ali. ( Picha na Ofisiya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kitengo cha habari.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Othman Masoud Othman, akiweka maji kumwagilia kwenye shimo la mti baada ya kupanda mche wa Mumbe katika hafla ya uzindizi wa upandaji miti Zanzibar . Hafla hiyo imefanyika leo tarehe 29/05/2022 huko skuli ya Mwera wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa Chuo cha  Zanzibar Microtech Bi Farhia Mohammed Ali. ( Picha na Ofisiya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar kitengo cha habari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad