HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 8, 2022

Vibanda 33 vimeteketea baada ya kuzuka kwa moto katika soko la Karume

 

Na Humphrey Shao,Michuzi Tv
VIBANDA 33 vimeteketea kwa moto baada ya kuzuka kwa moto katika soko lag Karume upande wa uwanja wa Karume ambapo wamiliki wake ni watu wenye ulemavu.

Akizungumza baada ya kufika katika eneo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija amesema taarifa ya tukio hilo alipata saa 11 alfajiri, ambapo vibanda hivyo vinauza mabegi.

Alisema kutokana na tukio hilo ataunda timu ya uchunguzi ambayo itafanya kazi kwa siku tano ambayo itatoka taarifa ili kuruhusu shughuli za wafanyabiashara hao kuendelea.

" Zipo taarifa kuna mwananchi anayeunganisha umeme kwa wafanyabiashara kinyume na taratibu , hivyo naagiza Jeshi la Polisi limsake au ajisalimishe," alisema.

Alisema hata hivyo timu atakayoiteua ikifanya uchunguzi itatoa maelezo ya kina kuhusu mtu huyo ili kujua kama ana kibali kutoka Tanesco ama vinginevyo.

"Inasemekana mtu huyo mara kwa mara anakuwa akizuiwa , wafanyabiashara tujiepushe kuruhusu watu wasio na mamlaka ya kuunganisha umeme," alisema.

Awali Mwenyekiti wa Walemavu katika soko hilo, Juma Malecha alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa wameshatoa taarifa za mtu huyo anayeunganishia watu umeme anayejulikana kama Mpemba kwa Tanesco kwa kuwa walikuwa na wasiwasi kuhusu ujuzi alionao.

"Mpemba au Mzee Shaha jana (juzi), alizuiwa kusambaza umeme . Hapa kuna tatizo tutakaa na Tanesco kuona kwa nini wamemrudisha," alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye Naye ameunguliwa na kibanda chake cha vinywaji na mabegi alisema kama viongozi alikataamtu huyo asiruhusiwe kuingizia wafanya biashara umeme.

Alisema kabla ya moto huo kuwaka, umeme ulikuwa umekatika uliporudi ndio moto huo ukatokea.

Alisema aliruhusu kwa walinzi kuvunja baadhi ya vibanda kuokoa mali na kuzuia mali moto usisambae zaidi.

Alisema baadhi ya mabegi yaliokolewa na pia kulikuwa na watu wasio waaminifu ambao Jeshi la Polisi lilifika na kudhibiti hali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad