Kauli hiyo imetolewa na wataalamu wa masuala ya uchumi nabiashara barani Afrika,baada ya kuzungumza na uongozi waBenki ya CRDB. Benki hiyo katika miaka ya karibuniimeendelea kutanua huduma zake nje ya Tanzania.
Rais wa Chemba ya Biashara Afrika (AfBC).Dk Amany Asfourakiwa na ujumbe wake uliojumuisha viongozi kutoka chemba zaBurundi,Uganda, Zambia, Botswana, Rwanda, Ethiopia na Misriwalikuwa nchiniu kwa ziara maalumu.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CRDB Jijini Dar es Salaam jana, Dk Asfour aliipongeza benki hiyo kwajitihada za kufungua milango na kuimarisha biashara kwenyenchi hizo.
Alisema mkakati wa CRDB kuziunganisha kibiashara nchi zaukanda wa Afrika Mashariki, unaendana na jitihada za viongoziwa mataifa hayo ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
“Hatua ya CRDB kutoa huduma nchini DRC ni kuonyesha kwavitendo jitihada za kuimarisha biashara baina ya nchi za ukandahuu na kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika utekelezaji wamkataba wa makubaliano ya eneo Huru la Biashara BaraniAfrika (AFTA)," alisema Dk Asfour.
"Nimefurahi kusikia CRDB inafungua kampuni yake tanzunchini DRC itakayokuwa na makao yake makuu mjiniLubumbashi. Hatua hii pia itachangia kukuza biashara baina yaBurundi, DRC, Tanzania," alisema Nshirimimana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliushukuru ujumbe huo kwa kutembelea nchini nakuwahakikishia kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana nawadau wa maendeleo wa nchi zote za ukanda wa AfrikaMashariki.
Nsekela alisema lengo la benki hiyo ni kukuza biashara baina yamataifa ya Afrika Mashariki, huku akibainisha kuwa kuingiakwa nchi ya DRC katika jumuiya hiyo,kutasaidia kuufanyaukanda huu kuwa imara na shindani kibiashara.
Alisema benki hiyo itaendelea kutanua huduma zake kutokanana sera madhubuti za Serikali zinazohimiza kukuza uhusiano wakidiplomasia na kiuchumi kwa nchi majirani.
"Dhamira ya Rais wetu (Samia Suluhu Hassan) ni kuendeleakufungua milango na kukuza uhusiano wa kibiashara baina yanchi zetu za ukanda huu pamoja na majirani wengine, sisi kamabenki tumejipanga kuhakikisha tunashiriki kikamilifu, ikiwamokatika kufanikisha miradi ya pamoja," alisema
No comments:
Post a Comment