HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 5, 2022

NIMR, AGA KHAN WASAINI MKATABA, KUSHIRIKIANA KATIKA TAFITI ZA MAGONJWA YA BINADAMU


Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh wa wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam. 

Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh wakionesha mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu waliosaini leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya akizungumza wakati wa kusaini Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh akizungumza kabla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Aga Khan Dkt Harison Mtuwa akizungumza mara  baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh wakisaini Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam.

Baadhi ya mashuhuda wa kusaini Mkataba wa Makubaliano katika tafiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam kati ya NIMR na Aga Khani.
Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano katika taiti za magonjwa ya binadamu leo  Aprili 5, 2022Dar es Salaam

*Wasaini Mkataba wa mashirikiano katika tafiti za magonjwa ya binadamu hasa yasiyoambukiza
* Kuwajengea uwezo wanafunzi wanaosoma Chuo cha Aga Khan

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR) wakishirikiana na Hospitali ya Aga Khana Dar es Salaam wamesaini Mkataba wa makubaliano ya kufanya utafiti kwaajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa mkataba wa makubaliano katika tafiti za magonjwa yote makubwa hata madogo.

"Tanzania sasa hivi kunaongezeko la magonjwa yasiyoambukiza na hayajafanyiwa tafiti, Taasisi ya Aga Khan teyari wanamradi mkubwa unaoendelea na wanafanya utafiti juu ya ugonjwa wa saratani Tanzania, hivyo wanafanya utafiti wa namna ya kuukabili ugonjwa huo." Amesema Profesa Mgaya.

Amesema ushirikiano huo utaweka nguvu ya pamoja katika eneo ambalo halijafanyiwa utafiti hasa la magonjwa yasiyoambukiza.

"Ushirikiano wa NIMR na Aga Khan iwe ni fursa ya kuwezesha kukabiliana katika kufanya tafiti na kuwa na ushahidi wa kutosha." Amebainisha Prof. Mgaya

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Sisawo Konteh, Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Aga Khan Dkt Harison Mtuwa amesema kuwa wanatambua NIMR kuwa na uzoefu mkubwa katika Tafiti za magonjwa ya binadamu hivyo wameona fursa hiyo na kufanya makubaliano katika kufanya tafiti za magonjwa ya binadamu hasa magonjwa yasiyo ambukizwa.

"Na kwetu sisi Aga Khan tumeona umhimu wa kuingia makubaliano na NIMR na sisi tunaanza kujifunza na kuongeza tafiti zinazofaa kwa Tanzania." Amesema Dkt. Mtuwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad