HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2022

Avunjwa miguu na mikono baada ya kufamaniwa na binti wa watu

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe
KIJANA anayefahamika kwa jina Benard Mkolwe mkazi wa kata ya Madilu,wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,amepigwa na kuvunjwa mikono na miguu baada ya kukutwa na msichana Sara Mgohole anayedaiwa kukutana naye nyumbani kwao kwa lengo la tendo la ndoa ikiwa ni siku ya kwanza tangu waanze mahusiano wiki mbili zilizopita.

Kijana huyo amekili kuwa na mahusiano na msichana huyo na kudai kuwa mahusiano yao yalikuwa yakuwasiliana kwa simu pekee na yana muda wa wiki mbili toka wayaanzishe hivyo siku ya tukio hilo ilikuwa ni siku yao ya kwanza kukutana kwa lengo la kufanya tendo la ndoa.

“Wakati wananipiga wakaniambia kwanini unatembea na binti yetu nikawaomba samahani nimekosa lakini hawakutaka kunielewa”alisema Benard Mkolwe

“Waliofanya tukio ni baba zake wadogo wa yule binti yule binti ni kama wiki mbili tuko kwenye mahusiano lakini sijawahi kufanya kitu chochote kile tulikuwa ni marafiki wa kuchati na ile siku alivoniita nahisi ndio ilikuwa siku ya kuelekea kwenye tendo lakini sikufanya kitu chochote”aliongeza Mkolwe

Kijana huyo anafanyiwa matibabu katika hospitali ya St. Jon's huku Daktari wa zamu wa hospitali hiyo Zainabu Said akieleza kuwa kijana huyo ameumizwa na sasa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo sambamba na kupinga vikali vitendo vya wananchi kujichulia sheria mkononi.

“Labda kuna visa vya awali huu ni ukatili wa kijinsia unaotokana na binti kusuka mpango kumuonea huyu kijana,yeye amekubali kuchati halafu wanakuja kumpiga na kama alikuwa hana uhitaji wa kukutana na huyu kijana angemkatalia toka mwanzo”alisema Tsere


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad