HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2022

UTEUZI; RAIS AWATEUA HAWA KUWA WENYEVITI WA TAASISI TOFAUTI

 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bibi. Sophia Mathayo Simba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jami (ISW). Bibi Simba ni Mbunge Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amemteua Jaji Hamisa Hamisi Kalombola kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma. Jaji Kalombola ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Amemteua Bw. Obey Nkya Assery kuwa Mwenyikiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC). Bw. Assery ni Mshauri Mwandamizi, Taasisi ya Global Alliance for Improved Nutrition, Dar es Salaam.

Uteuzi huu unaanza mara moja.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad