HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2022

WATU WASIOAHAMIKA WAUA MMOJA MADABA

 

Inocenti mwageni(72) mkazi wa kijiji cha mwande kata ya mateteleka halamshauri ya wilaya ya madaba amekutwa akiwa ameuwawa ndani ya kibanda chake kisha kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguu wa kushoto na watu wasiofahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Joseph konyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea aprili 12 mwaka huu katika eneo la mashambani vijijini mwande ambapo inadaiwa kuwa mwageni akiwa na mke wake Bonitha danda (65 ) waliondoka nyumbani kwao na kwenda shambani april 11 mwaka huu majira ya asubuhi kwaajili ya kwenda kulima na kupanda maharage ambapo mwage na mke wake walifikia kwenye kibanda chao kilichopo pembeni mwa shamba lao ambacho ukitumia kwa makazi wanapokuwa shambani.

Alisema kuwa mwageni na mke wake bonitha walifanya kazi hadi majira ya saa 11 jioni kisha walilejea kwenye kibanda chao pale shambani kwa kuwa waliishiwa mbegu za maharage za kupanda,mwageni alimwambia mke wake aende nyumbani kwao akachukue mbegu wakati huo mwageni akaamua kwenda kugema ulanzi na mke wa mwageni aliondoka na kumuacha mume wake pale shambani ila hakuweza kurejea pasipo kwa siku ile kwa ilikuwa ni usiku na giza lilikuwa limeingia hivyo aliona ni vyema kulala hadi asubuhi akiamini kuwa mume wake nae atalala kwenye kibanda cha shambani.

alisema kuwa ilipofika siku iliofuata asubuhi april 12 mke wa mwageni aliwahi kwenda shambani akiwa amebeba mbegu ya maharage na alipofika shambani ndipo alipogundua kuwa mume wake ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguu wa kushoto.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Konyo,alisema kuwa upelellezi kuhusiana na tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio ikiwa na pamoja na kuwasaka waliohusika na tukio la mauwaji ili sharia ichukue mkondo wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad