HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 11, 2022

SERIKALI KUTUMIA TRILIONI 41.9 BAJETI KUU 2022/2023

 

Janeth Raphael -  MichuziTv Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Mchemba amesema  kuwa katika mwaka 2022/23, Serikali inapanga kutumia  zaidi ya shilingi Tirioni  41.0 katika bajeti kuu ya serikali.

Ambapo amesema kuwa  Kati ya kiasi hicho, shilingi Tirioni 25.5 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni asilimia 62.2 ya bajeti yote, ikijumuisha shilingi Tirioni 11.3 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu na ambazo zimetengewa shilingi Tirioni 9.7 kwa ajili ya mishahara, ikijumuisha mapendekezo ya upandishaji madaraja na ajira mpya na shilingi Tirioni 4.4 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC). 

"Matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi Tirioni 15.5 sawa na asilimia 37.8 ya bajeti yote,Kati ya kiasi hicho, shilingi Tirioni 12.1 ni fedha za ndani, sawa na asilimia 78.1 ya bajeti ya 

maendeleo na shilingi Tirioni 3.3 ni fedha za nje,"alisema Waziri wa Fedha.

Ameekeza kuwa kwa kuzingatia sera, misingi, vigezo na vihatarishi vya bajeti, jumla ya shilingi Tirioni 41.3 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika, sawa na ongezeko la asilimia 8.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 2021/22 ya shilingi Tirioni 37.9.

"Jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi Tirioni 28.6 sawa na asilimia 69.9 ya bajeti yote,Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa

Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kuwa shilingi Tirioni 4.1 mwaka 2022/23, sawa na asilimia 10.1 ya bajeti yote,"amesema Dkt Mwigulu




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad