HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 11, 2022

PROF.NDALICHAKO AZINDUA BODI YA PSSSF


*Ampongeza Mhe. Rais kwa kuwezesha hatifungani kutolewa

*Bodi yaahidi kutekeleza majukuumu kwa uadilifu

*Asisitiza Uwekezaji uwe wenye tija na endelevu,

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemav, Profesa Joyce Ndalichako amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutolewa kwa hatifungani kama malipo ya deni la Serikali kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Profesa Ndalichako alisema hayo Ijumaa, Machi 11, 2022 jijini Arusha alipokuwa akizindua Bodi ya Wafadhamini ya PSSSF iliyoteuliwa Disemba mwaka jana.

“Tunamshuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha mwaka mmoja amewezesha kutoa trilioni 2.17 kwa ajili ya kulipa deni hilo lililodumu kwa muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi aliyoizindua, Mhe. Ndalichako alisema; “Natoa rai kwa Bodi kuhakikisha mnatekeleza majukumu yote. Nawapongeza kwa sababu Mfuko umeendelea kukua, naomba mhakikishe maswala yote ya fedha mnayasimamia vizuri ili tuweze kulipa mafao. Naomba mhakikishe mnawekeza kwenye miradi yenye tija”.

Akizumgumzia uwekezaji, Mheshimiwa Waziri alielekeza uwekezaji uwe kwenye miradi yenye tija na endelevu na Mfuko uendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kuwekeza kwenye viwanda vyenye uhakika wa kuongeza ajira na vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini.

“Nafahamu mnawekeza katika viwanda, mfano kiwanda cha Karanga (kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro), jana nilivaa viatu vya Karanga, ni vizuri sana, nawapongeza sana. Kiwanda hiki kitasaidia sana wafugaji wetu kuuza ngozi” alifafanua.

Kwa upande wa watumishi wa PSSSF, Mheshimiwa Waziri aliwataka kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili kufikia malengo yaliyopangwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alimpongeza, Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako kwa kuteuliwa na Rais, Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu

Akizungumzia utendaji wa Mfuko CPA Kashimba alisema tangu kuanzishwa kwake, Mfuko unatekeleza majukumu yake vyema chini ya usamimazi wa Bodi ya Wadhamini na kuongeza kuwa changamoto zilizokuwa katika mifuko iliyounganishwa zimefanyiwa kazi na sasa wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora kwa kiasi kikubwa.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa inajumuisha; Mhandisi Musa Iyombe ambaye ni Mwenyekiti, pamoja na wajumbe wengine ambao ni; Dkt. Aggrey K. Mlimuka, Bi. Suzan B. Kabogo, CPA Stella E. Katende, Bw. Victor F. Kategere, Bi. Mazoea Mwera, Bw. Thomas C. Manjati, Bw. Said A. Nzori na Bw. Rashid M. Mtima. Bodi ya Wadhamini ya PSSSF imeundwa kwa kuzingatia utatu wa uwakilishi kutoka Serikalini, Wafanyakazi na Waajiri.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa bodi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Musa Iyombe alisema, “Tunashukuru sana Mhe. Waziri kwa kuja kutufungulia, asante sana. Nakuhakikishia kazi ya Bodi ni kukushauri na maagizo yako yote sisi kama Bodi tutatekeleza pamoja na majukumu yetu kwa uaminifu na uadilifu, tupo makini hatutakuangusha.

Hafla ya uzinduzi wa Bodi ilihudhuriwa na; Profesa Jamal Adam Katundu, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad