Shule ya Academic Achievement ya jijini Dar e salaam imeeendesha mashindano ya vipaji na sayansi kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi
Akizungumza wakati wa maonyesho hayo Mkurugenzi wa Tasisi ya shule za Academic Achievement school, Abdullah Zakharia amesema lengo la kuendesha mashindano hayo nikujaribu kuvumbua vipaji kwa wanafunzi ambao wengine katika shule zao hawaja pata hizo fursa
Aidha amesisitiza kuwa wamezialika zaidi ya shule kumi za jijini Dar es salaa kwa ajili ya maonyesho hayo ya kazi za ubunifu kwa masomo ya sayansi
Baaddhi ya shule hizo ni Kinondoni, Kambangwa, Bunge Olimpio, Bunguruni Malapa na nyingine lengo likiwa ni kujaribu kuwakutanisha wanafunzi wenye mitizamo tofauti na wenye uwezo
Akifafanua zaidi alisema shule ya Academic inampango ya kufadhili wanafunzi wtakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi hivyo maonyesho haya yanaweza wanufaisha wanafunzi wanaosoma shule za kawaida za serikali .
Nae Mwanafunzi wa shule ya Bungoni alisema wao wamefurahi kuungana na wanafunzi ambao wanasoma michepuo ya kingereza lakini tulipofika katika swala la ubunifu woote tumekuwa tunaongea kitu kimoja tofautio yao na sisi wao wanauwezo wa kuongea Kingereza Zaidi yetu sisi tunaesoma katika shule za michepuo ya Kiswahili lakini nitajitahidi mwakani nishiriki kubuni kitu ili nipate ufadhili wa kusoma katika shule hizi.
Alli Sajjd akionyesha Robot la Umeme alilotengeneza kwa makatarasi na plastic kwa kutumia mfumo a umeme Jua wakati wa Mwanafunzi wa shule ya Academic achievement open school jijini Dar es salaam .Khalid Ramadhan Mwanafunzi wa shule ya Academic Achievement Open School akielezea jinsi alivyoweza kubuni na kutengeneza feni ya maboks kwa kutumia mfumo wa umeme na mabaki ya mabetri chakavu wakati wa maonyesho ya sayansna Ubunifu kwa wanafunzi wa shule msingi na sekondari .Mwanafunzi wa shule ya Academic achievement open school,Sumaiya Abdullwahd akielezea jinsi alivyoweza kutengeneza mfumo wa umeme kwa kutumia betri na na mionzi ya jua kwa wanafunzi ikiwa ni jaribio la sayansi wakati wa Maonyesho ya vipaji kwa masomo ya Sayansi yaliofayika shulerni kwao jijini Dar Salaam jana.Mwanafunzi wa shule ya Academic achievement open school,Malaika Sikandar akielezea jinsi alivyoweza kutengeneza mfumo wa umeme kwa kutumia mabaki ya betri na kuweza kuwasha taa kwa wanafunzi ikiwa ni jaribio la sayansi wakati wa Maonyesho ya vipaji kwa masomo ya Sayansi yaliofayika shulerni kwao jijini Dar Salaam.Kamati ya maandalizi ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikisha mashindano hayo
No comments:
Post a Comment