KARAHA YA UKOSEFU WA USAFIRI WA HARAKA MBAGALA KUBAKI HISTORIA MACHI 2023- DKT. MHEDE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 26, 2022

KARAHA YA UKOSEFU WA USAFIRI WA HARAKA MBAGALA KUBAKI HISTORIA MACHI 2023- DKT. MHEDE

 


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

SERIKALI iko mbioni kuwaondolea karaha ya Ukosefu wa huduma ya usafiri wa mabasi ya haraka kwa wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam ,ifikapo Mwezi Machi 2023 ,ambapo kwasasa mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu amefikia asilimia 44.4 .

Aidha  Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART ) unakwenda kuboresha miundombinu na Mazingira ya utoaji huduma kwa Kibaha na maeneo mengine ambayo mabasi hayo yameanza kutoa huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha baada ya kumaliza mafunzo ya wiki Saba ,kupitia wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara chini ya Taasisi zilizo chini yake Chuo cha elimu ya biashara (CBE ) na SIDO pamoja na kitengo Cha KAIZEN , Mtendaji Mkuu wa wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART)Dkt.Edwin Mhede alieleza, wakati wakitarajia ujenzi kukamilika, Mkandarasi atakapokabidhi na DART watakabidhi kwa mtoa huduma wa mabasi .

Dkt.Mhede alieleza, ujenzi huo ni ushirikiano wa Taasisi tatu ambapo Wakala wa barabara TANROADS wakiwa ni wasimamizi wa ujenzi wa miundombinu,UDART na Wizara mbili ya ofisi ya TAMISEMI na ujenzi ambao ni wasimamizi wa mradi.

"Licha ya mafanikio na changamoto ambavyo vilikuwa vinaonekana kwenye sekta yetu ya usafirishaji Wizara ya Uwekezaji ,Viwanda na biashara chini na Taasisi  ya CBE, SIDO na kitengo chake cha  KAIZEN imeona itushirikishe DART ione iliyofanya kwenye viwanda kama yanaweza kuleta tija na kwenye sekta yetu:"

:"Katika mafunzo tuliyoyapata tunahitaji kuwa na mabadiliko ya kifikra baina yetu DART na UDART tumekubaliana kufanya maboresho kwenye huduma zetu kuondoa karaha kwa wateja wetu wakiwemo wa ruti za Kibaha na maeneo mengine" alisema Dkt.Mhede.

"Tunakiri bado kuna uhitaji mkubwa wa mabasi kwa mkoa wa Dar es Salam peke yake japo ina magari mengi binafsi lakini inatoa asilimia 10 pekee ya mahitaji ya usafiri na asilimia 90 wanategemea usafiri wa umma" alisema Dkt Mhede.

Msimamizi wa Kitengo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Jane Lyatuu alisema mafunzo yametolewa kwa wiki Saba na yatakuwa endelevu.

Meneja upangaji ratiba na udhibiti kutoka kampuni ya mabasi yaendayo kasi UDART Daniel Madili alibainisha, kupitia mafunzo hayo wanakwenda kufanya maboresho kwenye huduma zao kwa wananchi.

Baadhi ya wakazi Kibaha , Loliondo akiwemo Josephine Dachi na Joseph Gabriel waliipongeza Serikali kwa kuwasogezea huduma ya mwendokasi hadi Kibaha.

Ila waliiomba chini ya DART kuwasogezea huduma hadi Kariakoo kwani wakifika Kimara wanapata shida.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad