Wanawake Wajasiriamali waifurahia Akaunti ya Niamoja ya Benki ya CRDB - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 23, 2022

Wanawake Wajasiriamali waifurahia Akaunti ya Niamoja ya Benki ya CRDB

Duniani kote, Wanawake wana mchango mkubwa sana katika jamii wanazoishi. Tafiti zinaonyesha wanawake wamepiga hatua kubwa katika kujitegemea kiuchumi na hivyo kupelekea kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya familia na shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.


Miriam Mdoe ni mmoja ya wanawake wajasiriamali ambao wana malengo makubwa katika biashara. Miriam ni mjasiriamali mwanamitindo wa mavazi, anasema safari ya ndoto zake ili anza pale alipojiunga na rafiki zake na kuanzisha kikundi cha kujiwekea akiba (VICOBA).

“Tokea nikiwa mdogo nilikuwa nikipenda kujishughulisha na ubunifu wa mavazi, nilipata ujuzi huu kupitia mama yangu ambaye alikuwa akishona nguo, nilitamani sana siku moja niwekeze katika biashara hii kwa kuwa na vifaa vya kisasa vitakavyoniwezesha kufanya biashara ya ushindani,” anasema Miriam.
Mariam anasema kuweka akiba kupitia kikundi kumemsaidia sana kuharakisha kufikia baadhi ya malengo yake ambayo amejiwekea ikiwamo kununua mashine za kisasa za kushonea na kuajiri mafundi wawili kwa kuanzia.

“Mnapoweka akiba kwa pamoja ni rahisi kufikia lengo kwa uharaka kwani kuna fursa ya kupata mkopo kwa ajili ya kujiendeleza,” anaelezea Mariam.

Mwanzoni walipoanza kuweka akiba walikuwa wakihifadhi fedha kupitia kibubu, hii iliwapa changamoto kubwa katika katika utunzaji wa fedha zao. Utunzaji wa kumbumbu ya michango na usalama wa fedha ulikuwa mdogo sana hadi pale mmoja wa rafiki yao alipowashauri wanakikundi wenzake kufungua akaunti ya Niamoja.

Mariam anasema kujiunga kwa kikundi chao na Akaunti ya Niamoja ya Benki ya CRDB kulifungua milango mingi ya mafanikio. Hii ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kuendesha kikundi chao kwa ufanisi wa hali ya juu na kufikia sehemu ya malengo yao waliyojiwekea.

“Akaunti ya Niamoja imetusaidia kuongeza usalama wa fedha na kutunza kumbukumbu sahihi za michango ya kikundi chetu. Kila mwezi tumekuwa tukipata taarifa ya kikundi inayotusaidia kufanya uhakiki wa michango, matumizi, mikopo kwa wanakikundi na mipango ya baadae,” anaelezea Miriam huku akibainisha akaunti hiyo ya Niamoja huwawezesha kupata taarifa ya akaunti bila makato yoyote.

“….. wakati tunafungua akaunti hii ilituhitaji kuwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi za Serikali, katiba ya kikundi na kianzio cha chini cha shilingi 20,000,” aliongezea Mariam.

Mbali na kikundi vya wajasiriamali binafsi kama wakina Mariam, Akaunti ya Niamoja pia hutoa fursa kwa vikundi vya familia na wafanyakazi kuweka akiba kwa pamoja. Hadi sasa akaunti ya NiaMoja ina vikundi zaidi ya 10,000 ikiwamo Vikundi vya Akiba na Mikopo (VICOBA), vikundi vya kuweka akiba vya familia na marafiki na vikundi vya upatu.

Pamoja na kuwa akaunti ya Niamoja inatumika na vikundi vyote, Mariam anasema akaunti hii imekuwa msaada mkubwa kwa wanawake kwa kuwainua kiuchumi kwa kuhamasisha uwekeji wa akiba.

“….. niipongeze Benki ya CRDB kwa ubunifu wa akaunti hii ambayo inatusaidia sana sisi wanawake, kwani pia inatufanya tutumie muda mwingi katika shughuli za maendeleo.  Wanachama wanaweza kutuma michango na marejesho ya mkopo kidijitali kupitia SimBanking, CRDB Wakala na hata kutoa benki nyengine na mitandao ya simu,” anasema Mariam huku akisisitiza kuwa mbali na kuweka akiba kupitia kikundi, vilevile amekuwa akijiweka akiba binafsi kupitia akaunti ya Malkia ya Benki ya CRDB ambayo ni maalum kwa ajili ya wanawake.

Akiongelea umuhimu wa huduma za kifedha katika kumuwezesha mwanamke, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema benki hiyo inachukulia kwa umuhimu sana suala la kujijenga kiuchumi kwa wanawake. Hii imepelekea kubuni huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kundi hilo la wateja. Huduma hizo ni pamoja na akaunti ya Niamoja, Malkia, Mikopo ya Wajasiriamali Wanawake (WAFI), pamoja na huduma nyengine za uwekaji akiba ikiwamo akaunti ya watoto ya Junior Jumbo.

“Mapema mwezi uliopita Benki yetu ilizindua kampeni maalum ya kuhamasisha wateja kuweka akiba ijulikanayo kama Jipe Tano, kampeni hii pia inalenga kuhamasisha wateja wanaoweka akiba kupitia vikundi ikiwa ni moja ya njia nzuri za kufikia malengo ama ya pamoja au ya mtu mmoja mmoja, na kama tunavyofahamu asilimia kubwa ya washiriki katika vikundi hivi vya akiba ni wanawake,” anasema Adili.

Adili anasema mpaka sasa Benki ya CRDB imeshatoa zawadi kwa wateja zaidi ya 1,000 katika kampeni ya Jipe Tano, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja kuendelea kujijengea utamaduni wa kuweka akiba ili kufikia malengo yao ya kimaisha.

“…. Tumetenga shilingi milioni 100 ambazo zinatolewa kwa washindi 240 kila siku, hivyo niendelee kuwahamasisha wateja waendelee kuweka akiba katika akaunti zao ili wapate nafasi ya kujishindia zaidi na wakati huo huo kutimiza malengo yao,” anasisitiza Adili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad