HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 23, 2022

TARURA, MANISPAA TEMEKE WAKUBALIANA MAPENDEKEZO RASIMU YA BAJETI YA BARABARA 2022/2023

 


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akiongoza kikao hicho cha mapitio ya rasimu ya bajeti ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa Manispaa ya Temeke.
Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Paul Mhere (kushoto) akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa uboreshaji wa barabara utafanyika katika kila Kata. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo.

Matukio wakati wa kikao hicho.


KIASI cha fedha cha zaidi ya shilingi bilioni 4 kimetengwa kwa ajili ya kutatua changamoto za miundombinu ya barabara za Manispaa ya Temeke katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Paul Mhere wakati wa kikao cha mapitio ya rasimu ya bajeti ya utekelezaji wa miradi ya barabara kilichowakutanisha Wakala hiyo kwa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo.

Mhere amesema, kiasi hicho kimetengwa ili kuondoa changamoto za ubovu wa barabara na kwa fedha hizo barabara zitajengwa kwa viwango vya changarawe, kuchongwa na lami.

Amesema kuwa hadi sasa wameshapokea bilioni moja kati ya nne na watahakikisha wanagusa barabara za Kata zote.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema fedha hizo zitakwenda kubadilisha mwonekano wa barabara za Manispaa hiyo ambazo nyingi zimekuwa hazipitiki hasa katika msimu wa mvua.

Pia Jokate amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.

Baadhi ya Madiwani wameipongeza TARURA kwa ushirikishwaji huo katika kupanga mipango ya Maendeleo na kuwapa nafasi ya kuwasilisha changamoto halisi za wananchi wa Kata zao.

Kikao hicho kilichowahusisha Madiwani kilimalizika kwa kuunga mkono mapendekezo hayo na kuboreshwa kwa baadhi ya mapendekezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad