Wadau
wa Afya wamekutana jijini Dar Es Salaam kufanya tathmini na kuweka
mikakati ya kuimarisha matumizi sahihi ya vituo vilivyoanzishwa kutoa
mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Afya kwa njia ya mtandao (Project -
ECHO), pamoja na kuendelea kufunga vifaa katika vituo vipya
vitakavyofunguliwa hivi karibuni katika Wilaya chache zilizosalia kupata
huduma hiyo.
Mpaka
sasa tayari vituo 265 vimeshaanzishwa nchi nzima na mikakati inaendelea
ya kuongeza vituo zaidi mikoa ya Kusini na Magharibi.Kikao hicho cha
wadau kimefadhiliwa na Serikali ya Marekeni kupitia mradi wa CDC
unaotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Mratibu
wa Mradi wa ECHO kitaifa (Project ECHO), Bw. Jacob Lusekelo
akiwasilisha ripoti ya tathmini wakati wa kikao cha wadau
walipokusanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Dr.
Idda Lyatonga, mmoja wa wataalamu wa tathimini na mratibu wa mpango wa
mafunzo kwa njia ya Mtandao (Project Echo) akichangia jambo kwenye kikao
cha wadau walipokutana Hoteli Sea Scape hivi karibuni.
Mtaalamu
wa Maabara kutoka TAMISEMI Bw. Alouis Nicas, akichangia jambo kuhusu
mafanikio ya mradi huo kwa wataalamu wa afya waliopo Wilayani baada ya
vituo kadhaa kufunguliwa na kuanza kutoka huduma.
No comments:
Post a Comment