RAIS SAMIA AMEIFUNGUA TANZANIA NA MKOA WA PWANI-RC KUNENGE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 17, 2022

RAIS SAMIA AMEIFUNGUA TANZANIA NA MKOA WA PWANI-RC KUNENGE

 


  Mhe Abubakar Kunenge ameeleza kuwa  Mhe Rais Samia Suluhu Hassan  amedhamiria kuhakisha kuwa anaboresha maisha ya Watanzania na kuondoa kero zao kwa kuleta Ustawi kwenye shughuli za kijamii na Kiuchumi. Ameyasema hayo leo Januari 16, 2022 wakati akikagua Daraja la Mbuchi  lililopo Wilayani Kibiti. 

"Tunajivunia Daraja hili la  Mbuchi linalojengwa kwa Gharama ya Shilingi Bilioni 6.245 litakuwa na urefu wa mita 61,  pamoja na Matengenezo ya Barabara hii ya Muhoro -Mbuchi- Mbwera ya urefu wa kilometa 23 kwa sasa Ujenzi umefikia asilimia 80". 

"Mhe Rais ameamua kuifungua Pwani kufika kusiko fikika" ameongeza kunenge.  

Kunenge ametaja kuwa uwepo wa Daraja hilo kutachochea shughuli za kiuchumi ikiwemo  utalii,Uvuvi na kilimo Biashara. 

ametoa rai kwa mkandarasi kufanya kazi usiku na Mchana na kukamilisha Ujenzi kwa wakati ifikapo Februari 23, 2022

Kunenge amewataka wananchi  kutojihusisha na Wizi wa vyuma vya Daraja hilo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad